Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako

Muhusiano ya mapenzi yanaweza kuanza vizuri, yakakua, na watu wanaopendana wakawa na ndoto kubwa kwenye mahusiano hayo. Lakini katika safari ya kuelekea kutimiza ndoto zao katika upendo au maisha ya kua pamoja, kuna mambo mengi hutokea na kuyumbisha mahusiano ya mapenzi. Baadhi ya mahusiano huwa yanadumu na kuendelea kusonga mbele pamoja na mambo mengi yanayoyumbisha.


Lakini pia Kuna mahusiano huwa yanavunjika na kushindwa kuendelea kusonga mbele kabisa. Kuvunjika kwa mahusiano huwa kunazalisha watu wenye mitazamo tofauti juu ya mapenzi na tabia tofauti pia. Hapa ndio utasikia “mapenzi ya kweli hamna… siji kupenda tena” na mambo mengine kama hayo. Mitazamo hiyo mara nyingi huja baada ya maumivu yaliosababishwa na kuachana. Maumivu baada ya kuvunjika kwa mahusiano yanaweza kukusukuma ufanye vitu vingi sana.

Japo kuachana na mpenzi hufanya mtu awe na maumivu lakini kuna vitu au mambo ambayo ni vema kuyaepuka.

Mambo ya kuepuka baada ya kuachana na Mpenzi wako

Kufanya vitu ili kumuumiza

Baada ya kuachana, kunaweza kuwa na mawazo mengi sana ya kukusukuma kufanya vitu vitakavyo muumiza mtu ulieachananae. Msukumo huu unaweza kukufanya usiwe makini na kupelekea ufanye maamuzi mabaya ambayo utayaona kama yanamuumiza lakini kwa upande mwingine yana haribu maisha yako wewe. Mfano mzuri ni kujihusisha na wapenzi wengi baada ya kuachana na Mpenzi uliempeda; unaweza hisi unamuumiza ulieachana nae kwa kumuonesha kuwa watu wengi wanakuhitaji lakini kwa upande mwingine ni maamuzi hatari kwako na sio kwake. Unaweza pata magonjwa, unaweza poteza muda wako na vuruga vitu vingine ulivyopanga kufanya maishani.

Kujilaumu au kumlaumu

Baada ya kuachana na Mpenzi wako unaweza kuwa ni mtu wa kujilaumu sana au kumlaumu ulieachana nae. Lakini kujilaumu au kumlaumu hakuwezi fanya kitu zaidi ya kukuletea maumivu pindi unapofikilia. Ni vema kujisamehe wewe na yeye pia alafu ukakubali hali na kuendeleza maisha yako. Chukulia kama yaliopita yote yalipangwa kuwa hivyo kwenye maisha yako na mambo mengi mazuri yanakuja mbele ya maisha yako. Usijishushe thamani kwaajili ya mtu asiyeona thamani yako. Wewe bado ni wathamani na unapaswa kujipenda na kujithamini hata kama umeachana na mtu unaempenda.

Kufuatilia mambo yake

Kufuatilia mambo ya mtu ulieachana nae, kunaweza fanya ukawa unaumia zaidi. Ni vema kama umeachana na mtu, ukaacha kumfuatilia mambo yake maana utakua unaumia pindi atakapokua anafanya vitu vinavyo uumiza moyo wako. Epuka kumfuatilia kwa siri maana utakua unatumia kwa siri hivyo hivyo.

Uamuzi mzuri wa kufanya baada ya kuachana na Mpenzi wako na kuona hakuna uwezo wa kurudiana ni kukubaliana na hali halisi, kujipenda na kuendelea na maisha yako mpaka utakapo taka kuingia kwenye mahusiano tena. Asante kwa muda uliotumia kusoma makala hii na natumaini umejifunza kitu. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi ya tuliozungumzia hapa.

Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook

Leave a comment