Kwenye simu huwa tunatuza namba na siku hizi Smartphone huturuhusu kutunza katika Email mbali na kuzitunza katika Laini na Simu yenyewe. Mara nyingi mtu unashariwa utunze namba za simu kwenye simu yako katika Email. Email ni sehemu nzuri ya kutunza namba zako maana huwa Inazitunza namba in cloud na kuzifanya iwe rahisi kuzipata hata utakapo ibiwa au kupoteza simu. Yani hata kama umeibiwa simu, ukiwa na taalifa za Email yako uliotunzia namba tu, unaweza ingiza email hiyo kwenye simu yako nyingine na ukapata namba za simu ulizotunza. Taalifa za Email tunazoziongelea ni Email yenyewe na Password yake tu.
Ukiona dalili hizi ujue akaunti yako ya Facebook si salama BONYEZA HAPA>>>
Katika ukurasa huu wa The bestgalaxy, hatuta zungumzia kuhusu utunzaji wa namba za simu zaidi ya hapa. Ila tunaenda kueleza jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika.
Jinsi ya kupata Namba za simu zilizofutika
Ikiwa umefuta namba yoyote kwenye simu yako na haipo tena kwenye Lain, Email na hata katika simu yenyewe, tambua bado unanafasi ya kuipata namba hiyo. Namba iliofutika kwenye simu inaweza kuwa katika akaunti yako ya Facebook iliopo kwenye app ya Facebook ya simu yako.
Ukiwa na app ya Facebook kwenye simu yako, huwa wanaomba ruhusa ya kuchukua namba za simu ulizotunza kwenye simu yako ili wazitumie kuiweka akaunti yako ya Facebook karibu na watu unaowajua. Hii ni moja ya sababu ambazo hupelekea kuwaona watu unaowajua kwenye Facebook.
Ukiruhusu ruhusu Facebook ichukue namba za simu kwenye simu yako, hata zikifutika kwenye simu, bado zitakuepo ndani ya akaunti yako ya Facebook. Kama uliiruhusu Facebook kuchukua namba za simu, unaweza fuata yafuatayo ili kupata Namba zilizofutika kwenye Simu yako.
- Ingia katika Facebook na ubonyeze vimistari vitatu gusa “Settings”
- Ingia kwenye settings alafu nenda kwenye “Accounts center”.
- Ingia kwenye “Your Information and permissions” na ubonyeze kwenye “Upload contacts”
- Chagua account yako ya Facebook utakayoiona Pele alafu utapelekwa kwenye ukurasa uliona orodha ya majina ya namba ambazo Facebook imeyatunza.
- Baada ya hapo utakua ukigusa tu majina ili kuona namba. Kwenye orodha ya namba hizo unaweza kuziona namba ya simu iliofutika kwenye simu yako.

Kama haukuiruhusu Facebook kuchukua namba za simu kwenye simu yako, unaweza usiikute namba ambayo unaihitaji. Ni hayo tu tulio kuandalia hapa ila usiache kutembea The bestgalaxy.