Athari za mwanaume kutumia pesa kutafuta mpenzi

Kwa sasa watu husema “Mapenzi ni pesa” na moja ya mambo ambayo huongelea ni kwamba ukiwa na pesa ni rahisi kupata mpenzi. Kwa wanaume, wanasema pesa inaweza kukufungulia mwanaume nguvu kubwa ya kuweza kuwavutia wanawake.
Na wewe ni mmoja kati ya watu wanao amini hayo? Sawa, ila ukweli ni kwamba pesa inaweza kufanya uvutie wanawake. Kuna wimbo wa zamani sana wa kiingereza wa Cyndi Lauper uitwao “Money Changes Everything”, yaani “Pesa hubadilisha kila kitu”. Wimbo huu kuna sehemu ni kama mwanamke anamuacha mwanaume wake na kuzifuta ahadi zote kisha kujielezea kwenye pesa huku akimwambia “…Tuliapishana upendo wa milele. Nilisema, ndio, najua, lakini tulipofanya hivyo, kulikuwa na jambo moja ambalo hatukuwa tukiwaza nalo ni pesa. Pesa hubadilisha kila kitu…”.

Wimbo wa Cyndi Lauper uitwao “Money Changes Everything”


Lakini sio wanawake wote hua hivyo, kuna wengine wamekulia katika hali za juu za kimaisha kiasi ambacho pesa haiwashtui sana na wengine wanawaogopa au wameisha fanyiwa vitu wasivyo penda na wanaume wenye pesa mpaka wakatenganisha mapenzi na pesa kwenye vichwa vyao.

Ukiwa mwanaume mwenye pesa na uwezo au mwanaume ambae hujifanya unapesa ili kuwakamata wanawake, hiyo inaweza kuwa ni njia rahisi kwako ya kuwavutia wanawake. Lakini njia hii ya kutumia pesa au kujifanya mwenye uwezo, inathari zake mnapokua kwenye mahusiano(au ndioa kabisa).

Athari 3 za mwanaume kutumia pesa kutafuta mpenzi

Kupotea kwa hisia za upendo.

Ukitumia pesa kumvutia mwanamke ambae anavutiwa na pesa au hali yako ya juu ya kimaisha unaweza jikuta unapoteza hisia za upendo mnapoendelea kuwa Katika mahusiano. Hii inaweza kutokea endapo mwanaume utatulia na kuona mwanamke amejisahau na kuweka mbele kukutoa pesa kuliko kuonesha upendo. Yani unaweza kufikia wakati ukaona kama hauna mwenza ila una mtu mnafanya nae biashara hivi na sio mahusiano. Hali hii inaweza fanya usijihisi kupendwa wala kupenda kabisa.

Kufilisika au kupoteza uwezo wako.

Mwanaume kutumia pesa kumvutia mwanamke ambae amevutiwa na pesa inaweza sababisha ukafirisika au kupoteza muelekeo wa kimaisha pindi mukiingia kwenye mahusiano. Hii inaweza tokea kama mwanamke atakua si mshauri mzuri au atakua mtu anae bomoa uwezo wako ili kujijenga yeye bila kujali chochote kuhusu wewe. Mbaya zaidi unaweza potea kimaisha alafu ukaachwa bila mwanamke huyo kujali hali yako.

Kunyanyaswa na kudanganywa.

Unaweza itumia pesa kuingia kwenye mahusiano na mtu asiekupenda kwa dhati na baada ya muda akachoka tu kukuigizia upendo pamoja na uwepo wa pesa. Hapa unaweza nyanyaswa kihisia au ukawa unadanganywa wazi wazi. Unaweza bambeleza sana mambo yawe mazuri lakini unakua haueleweki.

Mwisho; Sio Kila mwanamke unaempata kwa kuvutiwa na pesa au uwezo wako anaweza fanya mambo hayo. Ni baadhi tu ambao wako hivyo. Wanawake wengine unaweza kuwapata kwa kuvutiwa na pesa zako lakini wakakupenda na kuwa na mchango mkubwa katika maisha yako mukiwa kwenye mahusiano. Kikubwa ni kuwa makini ili kuepuka athari tulizo zungumzia. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.

Leave a comment