Mtandao wa instagram ni moja ya mitandao huwa inatajwa sana katika upande wa mitandao yenye kutumia sana data au bando la internet kwenye simu. Katika uzoefu wako wa kutumia mtandao huu kutoka Meta, unahisi unatumia sana bando la internet? Mh sijui kwa upande wako unawazo gani lakini ukweli ni kwamba mitandao ukiwemo instagarm ambayo hujihusisha na video huwa inatumia sana bando.
Instagram ina video ambazo hua zinajiplay bila hata uamuzi wa mtumiaji na video hizi hua zinachukua bando zinapojiplay. Mbali na video, picha zenye ubora pia zipo katika Instagram na picha zenye ubora hua zinachukua bando kuliko zisizo na ubora. Lakini hatuwezi sema mambo hayo kwenye instagram ni mabaya maana ndio kati ya mambo hufanya mtu ufurahie kutumia mtandao huu. Kama jambo la bando linakuumiza sana unawezafanya yafuatayo kutumia bando kidogo unapokua Instagram.
WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>
Jinsi ya kutumia bando kidogo unapokua Instagram
Njia rahisi na rasmi ya kupunguza matumizi ya data au bando lako la internet ni kutumia App ya Instagram Lite. App ya Instagam Lite ni app ambayo imeundwa tofauti na jinsi ilivyo App ya Instagram ya kawaida. App hii ni ndogo kuliko app ya kawaida na imepunguzwa baadhi ya mambo au vipengele ambavyo hutumia bando lako ikiwemo ubora wa picha na video . Hivyo, unapoitumia app ya Instagram Lite unakua unatumia bando kidogo kuliko ambavyo ungetumia app ya Instagram ya kawaida. Haitumi bando lako sana app hii na inaweza fanya vizuri hata kama mtandao wa internet kwenye simu yako haupo vizuri.

Kama hautataka kutumia app ya Instagram lite basi ni unaweza punguza matumizi ya data kwa kuwasha kipengele cha Data saver ambacho hupatika kwenye app ya Instagram ya kawaida. Kuwasha kipengele hiki, gusa vimistari vitatu vilivyo juu upande wa profile yako ya Instagram. Baada ya hapo ingia kwenye “Data usage and media quality” na uwase sehemu ya Data saver utakayoiona hapo.
Mbali na njia hiyo, unaweza punguza pia idadi ya video unazoangalia au ukapunguza muda unaotumia katika mtandao huu ili kupunguza matumizi ya bando lako.
Katika matumizi yako ya simu usifanye vitu hivi GUSA HAPA>>>