Kubembeleza mpenzi wako sio kuwa mjinga. Ni moja katika ya mambo muhimu kufanya unapokua kwenye mahusiano ya mapenzi na mtu anaekupenda. Na kubembeleza hua kuna nyakati zake na sio kila wakati. Unaweza hitajika kumbembeleza mpenzi wako baada ya tukio lililomuumiza hisia zake, baada ya kuchukizwa, kuonesha hali ya kukataa jambo unalohitaji au unapohitaji kumtuliza moyo wake na kumuweka sawa katika penzi lenu.
Kuna baadhi ya watu husema “mimi sjui kubembeleza kwenye mapenzi” au “mimi siwezi kubembeleza kwenye mapenzi” lakini unapaswa kufahamu kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kubembeleza hawaujui.
Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>
Kubembeleza mpenzi wako huonyesha upendo na kujali kwako kwake. Yani kunajinsi anahisi unamjali. Kubembeleza mpenzi wako pia kunaweza kuimarisha uhusiano wenu kwa kufanya muwe na maelewano ya amani. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kukuza uhusiano wa kimwili na kihisia kati ya wewe na mpenzi wako. Kubembeleza mpenzi wako kunaweza kusaidia kujenga imani kati yenu pia.
Huo ni muhimu wa kubembeleza katika mahusiano ya mapenzi ila kabla hatujaendelea, ukizidi sana kubembeleza inaweza kuwa sio jambo zuri tena. Lakini katika ukurasa huu tunaenda kuangalia sms za kubembeleza mpenzi.
Kutokana na utandawazi, watu hutumia sms kuwasiliana na wapenzi wao. Sasa ukiwa mmoja wa watu hawa, kuna sms ambazo mtu unaweza mtumia mpenzi kubembeleza kwenye mambo mbali mbali kwenye mahusiano yenu. Sms hizo unaweza tulia na kuziandika mwenyewe au unaweza angalia sms zitakazo kufaa hapa chini na kuzitumia.
Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>
Sms za kubembeleza mpenzi wako
- Wewe ndiye wangu mahabuba unaejua kunipa huba. Mwanamke ambae moyo umeushika. Nitabaki na wewe milele, sitochoka kukupenda malaika.
- Kuna muda nakaa nawaza jinsi gani naweza fanya ili nioneshe moyo wangu unakupenda kiasi gani ili tu uondoe mashaka juu ya upendo wangu kwako kipenzi. Natamani hata kukupeleka kwa wangu wazazi. Nakupenda sana mpenzi.
- Usije choka kunipenda honey. Na mimi siwezi choka kukupenda pia. Siwezi hata kuelezea jinsi nafurahi kuwa na wewe dear. Ninapokwambia “nakupenda” moyo wangu ndio unanituma kukuambia.
- Amini kuwa mimi nakupenda wewe japo wanaonitamani ni wengi. Moyoni mwangu kuna chumba chako wewe, sina vyumba vya wengi na humo upo wewe tu mpenzi.
- Tumekua hatuelewani sana katika siku hizi. Yawezekana ni shetani amekuja kutuchezea. Hebu tumshinde kwa kuanza siku ya leo vizuri kipenzi. Pamoja na yote tunayopitia, tambua sitamani kukupoteza. Moyo wangu bado unakupenda.
- Nisikupende wewe ili nimpende nani kwenye hii Dunia? Kuwa na wewe ni ndoto niliokua nasubiri kutimiza hapa chini ya jua. Hakuna anaeweza kuniamsha kwenye ndoto hii zaidi yako. Na sitamani itokee maana nakupenda sana.
- Ivi katika maisha yako umewahi ona penzi lililodumu kwa kusikiliza sana maneno ya watu? Mimi sijawahi, ila nimeona watu wanaodumu kwa kusikilizana tu. Hebu tupuuze ya watu twende mbele mpenzi wangu, nakupenda wewe tu.
- Nyakati za usiku wewe hua mwezi na wakati wa mchana wewe unakua jua langu. Kiufupi umekua msaada kila wakati ili nisipote kwenye giza. Nakupenda sana mpenzi.
- Wewe ni wapeke maishani na ninakupenda, sifikirii kukusaliti na wala sifikirii kukutenda. Nakuomba tuendelee kupendana kila siku siku habbity wangu.
- Unataka kuondoka kwenda wapi? Unataka kunicha na nani mwenzio? Unataka kuniumiza kweli? Atatibu nani majeraha unayota kuniachia? Hebu tumia dakika chache kufikilia tulipotokea. Kumbuka kuwa nakupenda sana mpenzi wangu.
Mwisho; Sms hizi zinaweza tumika na wanawake au wanaume. Kikubwa unapotumia, hakikisha inaendana na hali yenu ya mahusiano au mazungumzo.
