PUBG Mobile ni Game linalokutupa katika eneo moja uwe kati ya wachezaji 100 wanao pambana kubaki hai katika eneo hilo. Gemu hili linachezwa na watu wengi sana hapa Duniani pamoja na kuzuiliwa kwenye baadhi ya nchi.
Mechi moja ya PUBG inaweza kuwa ngumu au nyepesi kwako maana unacheza na watu halisi unaoweza kutana nao alafu ukawazidi uwezo au wakakuzidi uwezo. Kiufupi ni ngumu sana kuwa mtu unaweza kumzidi kila unaekutana nae kwenye mechi ya gemu la PUBG. Kuna muda ukiwa kama mchezaji unaweza jikuta umefanya vibaya kwenye mechi na kutolewa kwenye mechi mapema.
Kuishi muda mrefu katika mechi ya game la PUBG ni jambo muhumu sana na hutoa points za uhakika. Hata usipokua na Eliminations nyingi, ukiishi kwa muda mrefu kwenye mechi utapewa points.
Kama umekua na changamoto ya kutoishi muda mrefu katika mechi ya game la PUBG, yafuatayo ni mambo yanayoweza kukufanya ukishi muda mrefu kwa urahisi kidogo.

Mambo ya kuzingatia kuishi muda mrefu katika mechi ya game la PUBG
Chukua Level three helmet
Unapotua na kukusanya vitu katika mechi ya PUBG, huwa ni ngumu kupata kitu unacho hitaji maana vitu huwa haviwi kwenye mpangilio unaoeleweka. Lakini kama utabahatika kupata “Level three helmet” usiiache. Level three helmet katika mechi ya PUBG hulinda zaidi kichwa chako pindi kinapo pigwa na maandui. Level three helmet inaweza kulinda kichwa chako hata ukipigwa na M24 ambayo watu huiogopa pindi inapo nguruma katika eneo.
Usitembee kwenye sehemu za wazi
Hata sehemu iwe inaonekana salama kiasi gani, hakikisha haupiti bila kuwaza utajificha wapi pindi utakapo sikia mtu kaanza kukushambulia. Ukiwa unapita sehemu ya uwazi katika gemu la PUBG ni rahisi mtu usiemuona kukuona wewe na kuanza kukushambulia. Hivyo ni vema ukawa na tabia ya kupita sehemu zisizo na uwazi ili usipoteze maisha mapema. Pendelea kupita sehemu zenye mawe makubwa, miti, majani marefu au nyumba ili kuishi mda mrefu katika mechi ya game la PUBG.
Usikimbilie Eliminations kuliko kulinda uhai wako
Kutafuta Eliminations kwenye game la PUBG mobile ni kitu kizuri tu. Ila kama utakua unacheza ukiwa na tamaa ya kupata Eliminations nyingi alafu unasahau swala la kujilinda mwenyewe, utakua haudumu sana kwenye mechi. Kabla ya kufuata mtu kushambulia, hakikisha upo kwenye upo kwenye usalama na unauhakika wa kumuweza. Kama unaona upo kwenye hali mbaya, kujificha au kukimbia inaweza kuwa uamuzi mzuri pia.
Kuwa makini unapofuata Airdrops
Airdrops zinaposhuka huwa watu wengi wanaangalia juu ili wajue zinapotua. Zikishatua tu, kuna watu wengi wanakua tayari wapo njiani kuzifuata. Sasa ukiwa mmoja kati ya watu wanaozikimbilia Airdrops hakikisha unakua makini maana watu wengi wanaenda sehemu unayoenda. Mukikutana, wanaweza kukuzidi au ukawazidili lakini sehemu za Airdrops bado huwa ni hatari maana watu wengi hushindwa.
Usitue sehemu zenye majina makubwa mara kwa mara.
Kuna sehemu Katika ramani za game la PUBG mobile huwa zinafahamika sana. Watu wengi huwa wanapenda kushuka katika sehemu hizi kiasi kwamba unaweza tua na kupoteza maisha ndani ya sekunde chache tu. Sasa ukitaka kuishi mda mrefu katika mechi ya gemu la PUBG, usiwe na tabia ya kutua katika maneno haya. Tua katika maneno ambayo watu wengi hawatui ili upate hata muda wa kujiweka sawa.
Mwisho; Game la PUBG mobile ni gemu linalohitaji ujipe muda wa kujifunza pia. Jipe muda wa kucheza Kila mara ili upate uzoefu wa kulicheza na huu uzoefu unaweza kukufanya uwe na wezo wa kuishi mda mrefu katika mechi. Asante sana na endelea kuwa karibu na The bestgalaxy.