Mahusiano ya mapenzi yanaweza kuwa na vitu vingi vya kuongelea na hapa Kwenye ukurasa huu tumechagua kuzungumza mambo ya kuepuka katika mahusiano. Katika mahusiano, Kuna mambo usipo ya epuka yanaweza hatarisha mapenzi au mahusiano yenu. Mambo haya haijalishi ni mwanaume au mwanamke, ni vema kuyaepuka.
Mahusiano ni kama mmea unaouotesha aldhini na kuhakikisha kuna uwepo wa mambo yanayo ruhusu mmea huo kuota au kuendelea kukua na sio kufa. Lakini pia Kuna vitu pia unahitaji kuepuka kwenye mahusiano ya mapenzi ili yasife kama mmea.
Maneno ya kumwambia mpenzi wako usiku BONYEZA HAPA>>>
Mambo muhimu ya kuepuka katika mahusiano (wanawake na wanaume)
Kupoteza Imani
Uaminifu unatakiwa kuwa ni kati ya vitu muhimu sana katika kustawisha mahusiano. Pia uaminifu ni moja ya vitu ambayo sio rahisi kuvipata pindi mtu anapopoteza.
Kuaminiana kwenye mahusiano hufanya mahusiano ya mapenzi kuwa mazuri sana kwa wapenzi. Lakini endapo imani kati yao itatoweka, basi mahusiano yanaweza kuanza kuyumba hapo. Kama upo kwenye mahusiano na mpenzi wako ni vema kutunza na kuiheshimu imani ya mwenza wako kwako. Epuka kutumia imani yake kwako kumdanganya au kumuona mjinga siku imani ikitoweka, hata neno “Samahani” linaweza kuwa halina uzito.
Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>
Kukata Mawasiliano kati yenu
Mawasiliano pia husemwa kuwa ni moja kati ya vitu muhimu kwenye mahusiano ya mapenzi. Ni kweli mahusiano ni jambo muhumu na endapo mawasiliano yatafifia au kukatika katika mahusiano ya mapenzi, Unaweza kuwa ndio mwanzo wa mahusiano kuisha. Epuka kukata mahusiano kati ya wewe na mpenzi wako maana unaweza kuwa ndio mwisho wenu.
Kushusha heshima na kuiinua dharau.
Unaweza kuwa na mahusiano na mtu, mmezoeana sana kiasi kwamba unajua vitu vyake vingi sana vizuri na vibaya. Hata ujue sana, haushauriwi kushusha heshima na kuinua dharau. Kama kuna mambo ya kumsaidia, msaidie tu bila kumdharau. Kama kuna vitu vya kumvumilia, mvumilie bila kumuonesha dharau. Epuka kumtukana, kumsema vibaya kwa watu au kutomsikiluza. Ziheshimu hisia zake na kujali upendo wake kwako.
Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>
Kukosa Malengo
Mahusiano huwa na malengo pia. Mkishatulia kwenye mahusiano ni vema kuwa na malengo mnayojiwekea ili muishi kutimiza. Msipo kuwa na malengo kwenye mahusiano, mnaweza yumba kirahisi na kuachana kwasababu ya kukosa muelekeo. Malengo hufanya mahusiano ya mapenzi yawe na muelekeo. Malengo yanaweza kuwa ni mipango ya baadaye kama vile ndoa, familia, au malengo ya kifedha katika maisha yenu.
Kuingiliana kwenye mambo mengine
Wapenzi katika mahusiano huondoleana mipaka mingi sana. Lakini unapaswa kufahamu kuwa kuna baadhi ya vitu au mambo ukiwa kwenye mahusiano unashariwa kutoingilia. Kama kuna mambo yake au vitu anapenda na haviathiri mahusiano au maisha yenu, ni vema kuishia kuwa mshauri tu au kutomuingilia kabisa. Upuka kumuingilia kwenye mambo yake binafsi.
Mwisho; mambo yote tulio ya zungumzia hapa, yana umuhimu mkubwa katika mahusiano. Hatakama kutakua na changamoto katika kuyazingatia, ni vema ukapambana na kuanza kuyazingatia ukiwa kama mwanamke au mwanaume.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook