Mara nyingi watu, hutumia simu walizonunua alafu hununua nyingine mpya baada ya muda flani. Sababu za kununua hutofautiana maana kila mtu huwa na jambo lake liliomsukuma kutoa pesa yake na kunua simu mpya. Kuna watu hununua simu mpya baada ya kuona simu ya zamani imeharibika kabisa, wengine hununua baada ya kupoteza simu, pia kuna wengine huwa wananuanua simu mpya kutokana na kuichoka simu ya zamani au kutamani kubadilisha simu tu.
Kama unatabia ya kununua simu mpaya ili kubadilisha simu au kwenda na wakati ni jambo zuri. Simu mpya huwa zinakuja na maboresho pamoja vitu vingine vizuri kwa huo wakati zinaotolewa. Hivyo kwenda na wakati katika upande wa simu ni jambo zuri. Lakini unaponunua simu, mpya simu ya zamani huwa unafanya nini?
Kama haujui matumizi ya simu yako ya zamani unapo nunua simu mpya, soma hapa chini ili kufahamu jinsi wanavyoweza itumia.

Matumizi ya simu ya zamani unapo nunua mpya
Badili kuwa kifaa cha games
Simu yako ya zamani kama ipo vizuri na inaweza kuwekwa games za kucheza, basi ibadili kuwa kifaa cha games. Kuna games nzuri sana ambazo unaweza zijaza kwenye simu hiyo alafu ukitulia ukawa unazicheza. Sio lazima iwe wewe tu unacheza, hata ukiwapa watoto inaweza kuwa vizuri pia.
Ifanye WiFi ya nyumbani
Simu za smartphone huwa zina WiFi ambayo unaweza unganisha vifaa vingine vinavyotumia internet alafu vikatumia internet kupitia simu hiyo. Sasa endapo itakua na simu ya zamani na laini ya simu usioitumia, unaweza weka bando la kutosha kwenye hiyo laini alafu ukiingiza kwenye simu kisha ukawa unaitumia iyo simu kama WiFi ya nyumbani kwako. Kama unatumia internet kwenye PC au simu yako, hii inaweza kuwa nzuri kwako maana utakua unaiunganisha kifaa chako kwenye simu hiyo ya zamani ili kupata internet.
Iweke kuwa simu ya nyumbani
Unasimu ambayo ukiwa mbali na nyumbani ukiipiga mtu yoyote aliopo nyumbani anaweza ipokea? Mh sawa. Ni vema kuwa na simu ya nyumbani ili ukipata dharura au wakipata dharaura watu alioko nyumbani muwasiliane. Kama hauna simu ya zamani, unaweza ibadili kuwa simu ya nyumbani kwa kuiwekea laini na kuwaambia wanaoshinda nyumbani waitumie kama simu ya nyumbani tu.
Badili kuwa kifaa Cha Muziki na video
Kama unapenda kusikiliza nyimbo na kuangalia filamu, basi simu yako ya zamani inaweza kukufurahisha kwenye hilo. Unaweza ijaza nyimbo zote ambazo huwa ukitulia unazisikiliza sana bila kuchoka au ukajaza filamu unazozipenda sana. Baada ya kufanya hivyo ukipata muda utakua unachukua iyo simu na kusikiliza nyimbo au filamu zako bila Kuigusa simu yako mpya na kumaliza betri.
Tunzia file usizotaka kutembea nazo au zipotee
Simu yako ya zamani pia inaweza tumika kama kifaa cha kuhifadhia vitu vyako. Unaweza ingiza mafaili ambayo hautaki yapotee au hautaki yawe kwenye simu yako mpya. Ukishaingiza, unaweza ficha hiyo simu sehemu ambayo unahisi ni salama. Kama ni mtu unaekumbuka password, basi unaweza weka na password kwenye simu hiyo.
Unaponunua simu mpya, usisahau kuwa thamani ya simu ya zamani bado ipo. Kikubwa ujue jinsi gani utaitumia simu ya zamani baada ya kupata simu hiyo maana usipojua hautaiona thamani yake.
Mbali na yote, kuiuza au kuigawa ni jambo zuri pia maana unakua ni kama unawasaidia watu wengine kupata simu na kuwaonesha upendo.