Siku hizi Mapenzi ni Pesa au bado Upendo wa kweli upo?

Uhusiano wa pesa na mahusiano ya mapenzi umekua ukifanya watu wa wawe na imani tofauti kuhusu mapenzi ya sasa. Kuna watu wanaamini kuwa kwasasa mapenzi bila pesa ni hayapo. Na pia Kuna watu wanaamini kuwa mapenzi bila pesa yapo.


Ukweli usio fichika ni kwamba pesa imekua na umuhimu mkubwa sana katika maisha ya binadamu katika kipindi hiki. Japo sio yote, lakini mambo mengi katika maisha ya binadamu huwa yahitaji pesa ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Mapenzi na Pesa

Pesa juu ya Upendo wa kweli


Katika mapenzi, mara nyingi pesa inaanza kuwa juu ya upendo wa kweli kutokana na uhitaji wa vitu au maisha yanayo hitaji pesa. Pesa haiwezi kuendesha au kuvuruga mahusiano ya mapenzi kama watu au wapenzi watakua hawahitaji kufuata maisha au vitu vinavyo hitaji pesa nje ya upendo au mahusiano yao.

Kwa watu ambao huingia kwenye mahusiano yenye upendo wa kweli lakini wanahitaji sana vitu au maisha ya juu yalio nje ya upendo wao au mahusiano walionayo, ni rahisi kutupa chini ndoa au mahusiano walionayo na kuanzisha mahusiano na mtu mwenye pesa au maisha wanayohitaji.


Kuna wanaume wapo tayari kuacha mahusiano yao na kufuata mwanamke mwenye pesa na pia kuna wanawake wapo tayari kuacha mahusiano na kufuata mwanaume mwenye pesa. Hii haipo kijinsia kwa sasa.

Watu hawa wanaweza kuwa hivi kutokana na mazingira waliokulia, hali ya Maisha walionayo, tamaa au mitazamo yao juu ya mapenzi na pesa. Ukizungukwa au ukikutana na watu kama hawa kwenye mahusiano, inaweza kuwa ngumu kuamini kuwa kuna upendo wa kweli tena.

Upendo wa kweli upo

Mapenzi ya kweli yapo na yataendelea kuwepo japo watu hutoa hoja nyingi za kwamba mapenzi ni pesa kwa sasa, hasa katika mitandao ya kijamii. Lakini tukienda kwenye uhalisia, kuna watu wengi tu walipendana na wanapendana bila kuzingatia maswala ya pesa. Kuna watu wengi pia ambao wanapesa nyingi lakini upendo haupo kati yao kiasi kwamba wanaanza kutafuta watu wengine hata wasio na pesa ili kufurahia upendo. Kuna watu mpaka ambao hukataliwa na watu wanaowataka pamoja na kutanguliza pesa zao mbele, yani mtu anachukiwa yeye na pesa zake. Mbali na hayo, Kuna watu wengine hupendwa bila kuwa na pesa.


Ni ngumu kuuteka moyo wa mwanamke au mwanaume mwenye pesa kwa kumpa pesa ila kuna watu huuteka moyo wa mwanamke au mwanaume mwenye pesa kwa mapenzi.

Mambo hayo yanaweza kuwa yanaashiria nini? Hii ni ishara ya kwamba Mapenzi sio pesa japo pesa inaweza athiri upendo wa baadhi ya watu wanaokimbiza zaidi vitu vinavyo hitaji pesa au maisha yanayo hitaji pesa.

Mpenzi kuomba pesa

Jambo la muhimu la kujua hapa ni kwamba maisha ya sasa ya binadamu yanahitaji pesa ili kufanya baadhi ya mambo. Mukiwa kwenye mahusiano, ukiachana na Magari, maisha ya juu na zawadi za gharama, mpenzi wako anaweza kuwa na shinda au mahitaji ya muhimu yanayohitaji pesa. Kuombwa pesa za vitu kama hivyo na mpenzi wako haina maana mbaya na kumpa ni kumsaidia tu, sio ujinga.


Akikuomba pesa kwanini usimpe kama ipo ndani ya uwezo wako? Unaweza kumsaidia vipi hiyo shida yake bila kutumia pesa? Kuna sehemu nyingine unayohisi anaweza chukua pesa?

Kama unajua kabisa wewe ndie mtu wa karibu na jambo lake lipo ndani ya uwezo wako, shughulikia shinda yake maana upendo ni pamoja na kusaidiana kwenye vitu hivyo ukiwa ni mwanaume au mwanamke.

Usipoonesha msaada kwa mpenzi wako mwanamke kwenye vitu vidogo vidogo vya muhimu vinavyo hitaji pesa, unaweza kumuweka kwenye hatari ya kushawishika na kuanza kukimbilia pesa nje ya penzi lenu. Ukiona anashida nyingi muanzishie hata biashara au michezo ya pesa ili asiwe anakuomba omba pesa moja kwa moja na wewe uwe unasehemu ya kumfukuzia.

Mwisho; Upendo wa kweli upo na kama mahusiano yenu yametawaliwa na upendo wa kweli ni jambo zuri. Uvumilivu ni jambo la msingi sana ili kudumisha penzi lenu pale mnapokua na hamna pesa. Tambua kuwa hakuna alie kamilika. Kuacha upendo na kuikimbiza pesa kunaweza kukufanya uangukie sehemu nzuri au sehemu mbaya. Unaweza fanikiwa kupata pesa na vitu vyote ulivyo hitaji lakini ukakosa upendo wa kweli maana upendo sio pesa wala mali. Ukiachilia mbali kukosa furaha au upendo wa kweli, unaweza angukia kwenye magonjwa au kupotezewa muda kisha kuachwa.

Pamoja na yote, hatuwezi zuia mitazamo. Mtazamo wako ni upi kuhusu Pesa na mapenzi?

Leave a comment