WhatsApp inatuwezesha watu kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki mtandaoni. App hii ina vipegele vingi na moja kati ya vipengele vyake kuna kipengele kinaitwa “Link a device”. Kipengele hiki kinamuwezesha mtumiaji wa Whatsapp kuunganisha akaunti ya WhatsApp kwenye vifaa viwili mpaka vinne. Baada ya kuunganisha WhatsApp kwenye vifaa hivyo sms na vitu vingine vingi vitakua vinaonekana kwenye simu zote hata zikiwa mbali. Na kila kifaa kitakua na uwezo wa kutumika kujibu na hata kufuta sms.
Kama ni mtu mwenye simu mbili na unahitaji kuona sms zako za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa unaweza fanya hivyo kwa kutumia kipengele cha Whatsapp kiitwacho “Link a devices”. Hapa chini tunakupa mwanga juu ya jinsi unavyoweza kufanya kuungalisha na kuanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu nyingine bila kuigusa. Hakikisha hautumii kipengele hiki kialifu.
Jinsi ya kuunganisha na kuona sms za WhatsApp kwenye simu nyingine bila kuigusa
Chukua simu zote mbili za smartphone na uziunganishe kwenye internet(ziwe na bando). Simu yenyewe unataka kuangalizia sms tutaiita simu ya pili, simu ambayo ina sms unazotaka uwe unaziona tutaiita simu ya kwanza. Baada ya kuziweka sawa simu hizo, fuata yafuatayo:
- Chukua simu yenyewe unataka kuangalizia sms kwenye simu nyingine(simu ya pili) alafu ufungue web browser (Chrome) na kwenda katika website ya WhatsApp web ambayo ni https://web.whatsapp.com/
- Baada ya kufanya hivyo, washa “Desktop site” kwenye hiyo web browser.
- Baada ya kufanya hivyo, refresh ukurasa wa WhatsApp web alafu utaona kibox Cha QR code kimetokea kwenye ukurasa huo.
- Baada ya kufanya hayo kwenye simu yako ya pili, sasa uchukue simu yenyewe itakua na sms unazotaka kuziona(simu ya kwanza) kisha fungua app ya WhatsApp.
- Ukishafungua app ya WhatsApp, bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa juu alafu chagua “Linked devices”.
- Baada ya hapo utatupwa kwenye ukurasa wenye kitufe kilichoandikwa “Link a device”. Kibonyeze hicho kitufe alafu kamera ya simu hiyo itafunguka na utatakiwa kuitumia kamera hiyo kuscan QR code zinazooneshwa kwenye kile kibox kwenye simu nyingine. Ninaposema kuscan nnamaana elekeza hiyo kamera kwenye kibox kilichopo kwenye ukurasa wa WhatsApp web uliufungua kwenye ile simu nyingine.
- Ukisha scan itaunganisha akaunti hiyo ya Whatsapp alafu utaandika jina lolote la kwenye sehemu ya device name itakayo jitokeza uijaze na kusave.
- Baada ya hapo, utaanza kuona sms za Whatsapp kwenye simu zote mbili hata ukiwa mbali. Kiufupi utakua umefanikiwa kuziunganisha na utakua na uwezo wa kuangalia sms za Whatsapp za simu ya kwanza kwenye simu ya pili kupitia https://web.whatsapp.com/ ambayo ambayo inaitwa “WhatsApp web”.
- Yani ukitaka kuangalia sms za WhatsApp za simu nyingine bila kuigusa, utaingia https://web.whatsapp.com/ kupitia Web browser yako na kuwasha “Desktop site” kwenye hiyo web browser ( Chrome) bila kuscan tena mara ya pili.
- Ukifanya hivyo tu, moja kwa moja sms za simu ya kwanza utaziona kwenye simu ya pili kwa muonekano huu chini.

Hatua hizi zinaweza kuwa ngumu kama sio mtu unaejua sana vipengele vya simu. Lakini nadhani wengi wanaekewa vipengele vyote nilivyoelezea.
Mwisho; muunganiko huo utakatika endapo simu ya kwanza yenye sms itakua haijawa online kwa siku ya 14, ambazo ni sawa na wiki mbili.
Kuwa mjanja! Tufuate kwenye akaunti zetu mpya za kijamii ; Instagram na Facebook