Wanawake wanavutiwa na nini zaidi kwa wanaume

Mwanaume mara nyingi huwa ndio wanaonekana kuvutiwa na wanawake na sio wanawake wanavutiwa na wanaume. Lakini ukweli ni kwamba wanawake pia huvutiwa na wanaume japo hawana ujasili wa sema moja kwa moja kwa mwanaume kuwa kavutiwa nae.
Wanawake huwa wanavutiwa na wanaume na wengi wao wakitulia hukaa na kujadili wanaume wanao wapenda. Lakini wakikutana na hao wanaume wanao wapenda, ni ngumu kwa wao kuwa wazi kama jinsi wanaume wanavyo kuwa wazi wanapo kutana na wanawake wanao wapenda.


Hapa Kwenye ukurasa huu, The bestgalaxy tunaenda kukupa baadhi ya vitu au mambo wanawake wanavutiwa nayo zaidi kwa wanaume. Kuna vitu au mambo mengi wanawake wanaweza kuvutiwa nayo kwa mwanaume ila sisi hapa tumeeleza baadhi tu.

Mwanaume kuogopa wanawake wazuri kupita kiasi Fahamu kuhusu hii BONYEZA HAPA>>>

Wanawake wanavutiwa na nini zaidi kwa wanaume

Muonekano na harufu nzuri

Mwanaume mwenye muonekano mzuri huwa anawavutia wanawake. Lakini hapa swali ambalo linaluja ni “muonekano upi ni mzuri?”. Mwanaume msafi na anae vaa nguo zinazomkaa vizuri kuendana na mwili wake anaweza kuwavutia wanawake zaidi. Ndevu na nyele zilizo katika hali nzuri ya usafi huwafanya mwanaume awe na muonekano mzuri wa kuvutia wanawake.
Ukiachilia mbali mambo ya muonekano, harufu nzuri pia huwa inavutia wanawake. Tafiti nyingi zimekua zikionesha kuwa baadhi ya wanawake huwa wanavutiwa na harufu nzuri toka mwanaume.

Kuvutia kusomwa


Maisha ya binadamu ni kama simulizi inayoandikwa na watu wengine huwa wanasoma. Mambo mengi huwa tunasikia kuhusu watu kabla hatujakutananao na mambo haya huwa yanafanya tuwapende na tuwe na shauku ya kututana nao kabla hatuja kutana nao.
Sasa wanawake wanaweza kuvutiwa na mambo yako anayoyasikia alafu hata akikutana na wewe atatamani kuendelea kukujua na kukuosoma. Endapo ataendelea kugundua vitu vizuri kuhusu wewe, utamvutia kuendelea kukusoma na ndio basi utakua umemteka hivyo.

Kutokana na hili inashauriwa kutomwambia mwanamke mambo yote mazuri kuhusu wewe unapoingia nae kwenye mahusiano. Mambo mengi muache agundue mwenyewe au mwambie mbele ya safari.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Mwanaume anaejali na kuheshimu


Mwanamke anampenda mwanaume anaemjali. Kumjali ni jambo pana sana japo wengine huisi ni kumpa pesa na vitu vya thamani.
Mwanamke anampenda umjali kwa kumpa muda wako, kumsaidia kwenye baadhi ya mambo na kumuonesha tabia nyingine zinazoweza muaminisha kuwa yeye ni mwanamke unaemjali. Hatakama haupo nae kwenye mahusiano, kuna jinsi tu anaweza hisi unamjali na ukaugusa moyo wake akavutiwa na wewe japo ni ngumu kukuambia.

Ujasiri na msimamo

Wanaume wenye ujasiri na msimamo katika maisha yake anaweza vutia wanawake wengi sana. Unaweza onekana jasiri kwa mwanamke kwa kuchukua nafasi za uongozi, kuongea vizuri mbele ya watu, kuendesha maisha yako vizuri na kutatua changamoto mbalimbali. Msimamo katika mambo unayofanya inaweza mfanya avutiwe zaidi na wewe.

Vitu vya kushangaza ambavyo hutokea ukimpenda mpenzi wako sana BONYEZA HAPA>>>

Ucheshi na uwezo wa kujieleza

Wanawake mara nyingi huvutiwa na wanaume wenye hisia za ucheshi na uwezo wa kujieleza. Mwanaume ambae anaweza ongea na mwanamke vizuri na kumfurahisha au kumchangamsha kwa ucheshi wake, anaweza mvutia mwanamke kirahisi.


Ukiachilia mbali ucheshi, uwezo wa kujieleza unaweza fanya mwanamke akupende pia. Kunawezakuwa kujieleza hisia zako, kujitetea pindi unapokosea na mambo mengine kama hayo.

Mwisho; Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy ila kabla haujaondoka katika ukurasa huu, ni vema kutambua kwamba kila mwanamke anaweza kuwa na mambo binafsi anayovutiwa nayo kwa mwanaume.

Leave a comment