Apple vision pro: Fahamu kuhusu Miwani hii ya Apple

Miwani ya VR(VR headsets) ni vifaa vya kisasa ambayo huvaliwa na watu na hufanya watu kuanza kuona mazingira ya kisasa au yalioundwa tofauti na mazingira ya ulimwengu halisi. Ukivaa Miwani hii unaweza kuona upo kwenye ulimwengu mwingine kabisa na ulimwengu ulio uzoea alafu utakua na uwezo wa kufanya vitu katika ulimwengu huo.


Makampuni mengi hujihusisha na utengenezaji wa Miwani hii ya VR ikiwemo kampuni ya Apple inayotoa simu za iPhone. Katika February 2, 2024 huko US, kampuni ya Apple ilitoa Miwani ya VR itwayo Apple vision pro. Miwani hii ilikua ikisubiriwa sana na watu wanaofuatilia mambo ya VR maana ilikua ikiongelewa sifa na mambo ambayo itakua nayo kabla Apple hawajaitoa.

Mambo kuhusu Apple vision pro

Apple vision pro imebeba vingi vizuri

Kwasasa Miwani hii imeisha toka na unaweza ipata kama bidhaa nyingine za Apple tunazozifahamu kutoka kampuni Apple. Baada ya Miwani ya Apple vision pro kutoka kumekua na mambo mengine yameongelewa kuhusu badhaa hii ya Apple. Machache kati ya mambo hayo ni yafuatayo.

Apple vision pro Ina vitu vingi vizuri tunavyoweza viongelea. Kwanza kabisa Miwani hii ina “eye and hand tracking”. Kupitia hii unaweza ivaa na kugusa au kuchagua vitu unavyooneshwa na Miwani hiyo bila kutumia kifaa kingine. Unaweza kuchagua au kugusa vitu kwakutumia macho tu au mikono yako bila kuwa na kifaa kingine chochote mkononi.

Kwenye kioo, Apple vision pro Iko na micro-OLED displays zenye pixels milioni 23, ambazo zitafanya ufurahie ubora wa picha za 4k kwenye Kila jicho.
Kwa usaidizi wa kamera, Apple Vision Pro inaweza kuunda Avatar ambae ataonekana unapowapigia kupiga video call watu wengine kupitia Miwani hiyo.

Kiufupi, Apple vision pro ni bidhaa nzuri sana toka kampuni ya Apple na imetikisa ulimwengu wa bidhaa za VR katika mwanzo wa mwaka 2024. Angalia video hii hapa chini.

Video ya Apple vision pro

Bei


Moja katika ya vitu watu wameongelea sana baada ya Apple vision pro kutoka ni bei yake. Ukihitaji kununua bidhaa hii kutoka kampuni ya Apple kwasasa itakuhitaji uwe na $3,499. Hiyo ndio bei yake katika Dola za kimalekani, ukiigeuza kibongo bongo(Tsh) inaweza kuwa kama milioni 8 na laki 9 hivi.

Kuna baadhi ya watu ikiwemo CEO wa kampuni ya Meta, Mark Zuckerberg wamezungumza kuwa ni ghalama sana kuliko Miwani ya Meta Quest 3 inayofanya baadhi ya vitu kama Apple vision pro japo haina ubora sana kwenye baadhi ya vitu pia. Miwani ya Meta Quest 3 inapatikana kwa Dola 499.99 za kimalekani.

Lakini Kuna waataalamu wameeleza kuwa Apple vision pro imeundwa nah baadhi ya vitu vyenye gharama kuliko Meta Quest 3, hivyo inaweza kuwa ni sawa kuwa na gharama kubwa.

Credit: Apple

Haipo vizuri kwenye games

Baadhi ya watu wanonunua miwani ya VR huwa wanapenda kutumia zaidi upande wa games. Kucheza VR Games kwenye Miwani ya VR kunaweza huwa kunafurahisha sana. Sasa Apple vision pro bado haiko sawa katika upande huu.

Hand tracking yake haiko vizuri sana ukilinganisha na Meta Quest 3 na haina game nyingi za VR unazoweza furahia kuzicheza. Pia hand tracking haiko vizuri sana kiasi cha kukufanya ufurahie zaidi kucheza game za VR. Ila Meta Quest 3 ndio imetajwa kuwa vizuri katika upande huu wa games kuliko Apple vision pro.

Inaendelea kuboreshwa

Apple vision pro ni bidhaa nzuri Toka apple lakini ni toleo la kwanza, yani “first-generation product”. Mara nyingi bidhaa toleo la kwanza huwa zinakuja na matatizo na madogo madogo madogo ambayo kampuni huwa inaangalia namna ya kutatua na kuboreshwa bidhaa yao hiyo au zijazo. Apple vision pro nayo ipo kuboreshwa na kampuni ya Apple ili iweze kuwa bora zaidi.

Ni hayo TU katika ukurasa huu, usiache kuwa karibu na The bestgalaxy kwa mambo mengine zaidi.

Image credit: Apple

Leave a comment