Kulala na mme au mpenzi wa kiume katika chumba inaweza kuwa sio sawa na kulala peke yako. Kunaweza kuwa sio sawa kwasababu ya uwepo mtu anaekupenda katika chumba. Mtu huyo anaekupenda anaweza kukupenda jinsi ulivyo na mambo yako katika kulala lakini kuna mambo au vitu ukivizingatia unaweza ukamfurahisha zaidi anapolala na wewe chumba kimoja.
Unahitaji kumfurahisha mwenza wako wakati wa kulala usiku? Sawa, hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya mambo ya kuzingatia katika kulala na mme au mpenzi wako usiku. Tumia muda wako kusoma mambo haya hapa chini na kama kunakitu ulikua hukizingatii basi unaweza anza kukizingatia ili kumfurahisha mume au mpenzi munapolala wote usiku.
Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani BONYEZA HAPA>>>
Mambo ya kuzingatia katika kulala na mme au mpenzi wako usiku
Usafi
Hili tumeweka jambo la kwanza Kwasababu ni jambo muhumu sana. Usafi ukizingatiwa unaweza mfurahisha sana mme au mpenzi wa kiume katika kulala usiku. Tunapo zungumzia usafi, tunamaanisha Mwili unatakiwa kuwa msafi na pia chumba kinatakiwa kuwa kisafi. Hakikisha unaonga na sehemu zote za Mwili wako safi ikiwemo mdomo wako. Chumba chenu kifanye kiwe safi na kiwe kwenye mpangilio mzuri. Ondoa vitu vyenye harufu mbaya kisha ikiwezekana ongeza vitu vyenye harufu nzuri ya kumvutia. Kama chumba sio chako, yaani umemtembelea tu basi kuwa msafi wa Mwili wako inatosha.
Pozi la kulala
Huwa unalala mtindo gani ukiwa peke yako chumbani? Unahisi mtindo huo unaweza ruhusu mwema wako kulala vizuri mnapo lala wote? Kama haumruhusu kulala kwa uhuru kwenye kitanda, basi ni vema ukibadilisha mtindo huo ili kumfurahisha mume au mpenzi wako unapokua na usingizi. Unapojali usingizi wako, kumbuka kujali na usingizi wake pia kwa kulala vizuri usiku.
Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>
Nguo nyepesi
Ukiwa mwanamke, sio kila nguo inafaa kuvaa unapo lala na mtu wako usiku. Kuna nguo ambazo unatakiwa kuvaa na ukizivaa wakati wa kulala usiku, utamfurahisha mme au mpenzi wako wa kiume. Unashariwa kuvaa nguo nyepesi sana na ikiwezekana ziwe zinateleza kiasi, laini au fupi. Usivae nguo inaoufunga Mwili wako kama mzingo, jiachie bila kuona aibu.
Sauti na utulivu katika maongezi
Kama mtakua na maongezi kabla ya kulala basi sauti yako katika maongezi inatakiwa kuwa ya mahaba. Jitahidi uwe mtulivu na uongeaji wako usiwe wa dharau au kufokea. Maongezi ya usiku yanatakiwa kuwa ya kupendeza na wewe kama mwanamke ndio unaweza fanya yapendeze zaidi kwa kutoa sauti itakayo gusa moyo wa mwanaume wako huku mukiwa mnatafuta usingizi.
Ni hayo tu Katika ukurasa huu. Nafikili itakua ni vizuri ukiendelea kuwa karibu na The bestgalaxy ili kujifunza mambo mengine ukiachana mambo hayo.