Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu

Kama ni mpenzi wa magemu ya Xbox na una magemu yako pendwa ya xbox ambayo hua unayacheza kwenye vifaa vya xbox basi leo napenda kukufahamisha kuwa kuna uwezekano wa kuyacheza magemu hayo kwenye simu yako. Na hapa The Bestgalaxy tunaenda kukueleza njia ya kucheza game za xbox kwenye simu.

Haijalishi ni Simu ya Android au iOS(iPhone), njia inayoenda kuelezwa hapa inaweza tumika kwenye  simu hiyo vizuri tu ila inajumuisha malipo ya huduma.

Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu

Unaweza cheza magemu ya Xbox kwenye simu yako kwakutumia huduma ya Xbox cloud gaming. Huduma hii ni huduma ya Xbox inayowezesha watu kucheza magemu ya xbox na yasio ya Xbox kwenye simu kwa kutumia internet. Unaweza kucheza magemu hayo kwenye huduma hiyo bila kudownload. Kupitia huduma hii tunaweza sema sio lazima kununua kifaa cha xbox ndio ucheza magemu ya Xbox maana unaweza yacheza kwenye sumu yako kwakutumia internet kupitia huduma hiyo ya xbox cloud gaming..

Kujiunga na huduma ya Xbox cloud gaming ni bure kabisa ila baada ya kujiunga utakua na uwezo wa kucheza bure game la Fortine tu. Ili kucheza magemu mengine itabidi ulipie moja vifurushi vyao ambayo kwa mfumo wao huitwa “Xbox Game pass”. Kivurushi hivi huanza kwa bei ya ofa ya dola 1 tu kwa siku 14 alafu baada ya siku hizo kuisha utaendelea na malipo yao ya kawaida ya vifurushi.

Fuata hatua zifuatazo kucheza game za Xbox kwenye simu kwa huduma ya xbox cloud gaming.

  • Fungua VPN kisha uunganishe server ya USA kama haupo usa kwa sasa.
  • Ingia Google kwa web browser.
  • Tafuta “Xbox game pass” kisha ingia kwenye matokeo ya juu toka xbox.com
  • Baada ya kufanya hivyo, utatua kwenye ukarasa unaokukaribisha kujiunga kwa kuchukua moja ya vifurushi vyao kwa bei ya ofa. Bonyeza kitufe kilichoandikwa “JOIN FOR $1” kuanza taratibu za kujiunga.
  • Kabla ya kuendelea utapelekwa kwenye ukurasa wa kuingia na akaunti ya Microsoft au kutengeneza mpaya(kama hauna utatengeneza mpya na kama unayo utaiweka)
  • Chagua kifurushi chako cha “Ultimate” alafu bonyeza “Next” kuendelea mpaka kwenye ukurasa wa malipo kwaajili ya kulipia.
  • Ukisha lipia tu, utakua na uwezo wa kucheza magemu ya Xbox kwenye simu ndani ya hiyo huduma yao bila kudownload. Utakua unatumia mtandao tu.

Unapocheza magemu kwa njia ya cloud, ni vema ukawa na mtandao uliotulia sana maana hicho ndio kitu kikubwa kwenye kucheza magemu kwa njia hii. Endapo mtandao utakua haujatulia, game pia litakua linasumbua unapolicheza. Asante kwa muda wako, endelea kuwa na The bestgalaxy kwa mambo mengine mazuri.

One thought on “Jinsi ya kucheza game za Xbox kwenye simu”

Leave a comment