PUBG mobile ni game lenye jina kubwa katika ulimwengu wa magemu ya simu ya Battle Royale. Gemu hili huwakutanisha watu toka pande mbali mbali za dunia kama wachezaji wanao pambania ufalme wa vita.
Unapocheza game hili huwa unapata points ambazo zinakusaidia kuongezewa PUBG Ranks kwenye gemu hilo. PUBG Ranks zimepangwa Toka chini kwenda juu na kadri unavyoongezewa rank ndio unakutanishwa na watu wengine wenye uwezo mzuri kwenye gemu hilo. Ukishindwa kufanya vizuri katika mechi, unakatwa points na kushushwa Rank pia. Ace ni moja ya PUBG Ranks ambazo baadhi ya watu hukumbana na ugumu kidogo katika kuifikia.
Ikiwa upo hapa na unashindwa kufikia Ace katika gemu la PUBG, hapa chini Kuna mbinu chache ya kukusaidia kufikia Ace kirahisi.
Mbinu za kufikia Ace kirahisi kwenye PUBG
Ishi muda mrefu
Watu wengi huwa wanapocheza gemu la PUBG mobile huwa wanatafuta Eliminations nyingi. Ni jambo zuri lakini ukiwa na Eliminations nyingi katika mechi alafu haujaishi kwa muda mrefu, hauwezi pata points zitakazo kufanya upande Rank. Kudumu muda mrefu kwenye gemu ndio kitu cha msingi zaidi kwenye gemu na hukupa point nyingi za uhakika zitakazo kufikisha kwa haraka kwenye Ace. Usishambulie kuliko kujilinda. Jilinde usipoteze maisha kwenye game kwa kutua kwenye sehemu ambazo watu wengi hawatui, kuwa makini unapofuata airdrops na pia usisahau kuchagua siraha nzuri. Usiogope kuwa “lone wolf”.
Cheza mara nyingi
Kwakua mechi za PUBG huwa zinakupa points, basi ni vema kucheza mara nyingi maana kadri unavyocheza ndio unajizolea points zaidi ambazo zitakufanya ufikie Ace. Ukiachilia mbali Points, kucheza mara nyingi au mara kwa mara huongeza uzoefu ambao utakufanya ufanye vizuri kwenye mechi unazocheza.
Chukulia Ace ni kitu cha kawaida alafu zingatia points
Ace ni kawaida sana na kinachokufanya ufikie ni points. Sasa ni vema ukazingatia kupata point nyingi kwenye mechi zako na kuacha kuiogopa. Usichukulia kama ni kitu kikubwa sana, zingatia kwenye kuwa mchezaji mzuri kwenye mechi zako na kupata points nyingi alafu hizo points ndio zitaifikia Ace.

Mwisho; Fahamu kwamba kupata Ranks kubwa kwenye game la PUBG inaweza kuwa ni ngumu kwa baadhi ya watu kwasababu ya uzoefu. Ni vema kujipa muda wa kujifunza kutokana na makosa unayofanya kwenye gemu ili kupata uzoefu utakao kufanya mchezaji Bora.