Mambo 5 ya kuyajua unapotaka kumtongoza Mwanamke mtandaoni

Kutokana na teknolojia kuwaunganisha watu kupitia mitandao ya kijamii, watu wanaweza anzisha mahusiano ya mapenzi bila hata kuonana. Watu wengi tu hujikuta katika mahusiano ya mapenzi yalioanzia mitandaoni bila ya kuonana. Kuna mpaka ndoa ambazo zimefungwa zilizotokana na mahusiano yalioanzia mtandaoni bila kuonana.

Hapa kwenye ukurasa huu The bestgalaxy, tunaenda kukujuza mambo ya kuyajua mtu anapotaka mtongoza mwanamke mtandaoni. Hii ni kwaajili ya mwanaume ambae anataka kutupa kamba kwa mwanamke katika mitandao ya kijamii au app kama Facebook, WhatsApp, Instagram na Telegram. Unahitaji kujua mambo haya? Basi soma yafuatayo.

Jinsi ya kutunza mahusiano ya mbali BONYEZA HAPA>>>

Mambo ya kuyajua unapotaka kumtongoza mwanamke mtandaoni

Usitegeme kukufanyia mazuri maana hakujui.

Unapotaka kumtongoza mwanamke ambae hamjawahi kutana zaidi wewe kumuona mtandaoni, fahamu na kukubali kuwa hakujui. Kutokana na kutokukujua unaweza kutana na changamoto nyingi katika kuanzisha mahusiano. Anaweza kuwa hajibu ujumbe wako kwa wakati, anaweza kuwa mkali kwako, anaweza kuwa hajali hata kuondoka kwako kiasi kwamba anaweza kukublock muda wowote. Kiufupi usitegeme akufanyie mazuri maana hakujui sana kiasi cha kuzingatia au kujali hisia zako. Hii inaweza kuwa hata ni ishara ya kwamba unachati na mwanamke halisi na sio tapeli.

Unaweza kuwa si mmoja unaetuma ujumbe.

Kuna wanawake huwa ukiwatumia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, hawaonekani kusoma ujumbe kabisa. Kwa baadhi ya wanawake, hali hii inaweza sababishwa na kupokea ujumbe kutoka kwa watu wengi wasumbufu kiasi kwamba ujumbe wako haujaonekana au ameacha mazima kusoma jumbe zote zinatumwa na watu. Ukikutana na mwanamke wa namna hii, unaweza Endelea kumtumia ujumbe bila kukata tamaa au ukatafuta njia nyingine za kuwasiliana nae. Pia usisahau kuwa mbunifu ili kumvutia aendeleze maongezi na wewe.

SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>

Huangalia picha zako.

Ukifanikiwa kutumia ujumbe wa kwanza kwa mwanamke ulikutanane mtandaoni, unatakiwa kufahamu huwa akisha soma ujumbe wako, ataangalia picha zako kukujua. Kwa baadhi ya wanawake, picha zako zinaweza amua akujibu au asikijibu. Ukiwa na picha nzuri au unapost vitu vizuri, unaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuanza mazungumzo nae. Endapo endapo ni mtu unaepost vitu vya hovyo kama matusi au picha zinazomtisha, unaweza ukakosa bahati ya kuchati nae kabisa.

Unaweza muona tofauti mtakapo kutana.

Kama unapendelea kuchangua mwanamke kwa kuangalia picha zake, basi fahamu kwanza kuwa siku hizi picha zanaweza kuwa tofauti na uhalisia wa mtu. Picha zinaweza kupitia michakato mingi inayoweza fanya mwanamke anaeonekana kwenye picha awe tofauti kidogo na jinsi anavyoonekana kwenye uhalisia. Mara nyingi utofauti unakua ni mdogo na unatakiwa kujiandaa nao ili ukianzisha mahusiano na kukutana nae, usishangae sana.

Anaweza kukupenda pia

Mapenzi ya mitandaoni yanaweza kujengwa na kufikia hatua za ndoa. Unaweza pata mwanamke unaempenda mtandaoni, ukapambana kujuana nae, mukaingia kwenye mahusiano na akawa anakupenda toka moyoni pia. Jambo hili linawezekana ila epuka kuwa msumbufu kwake na uwe makini pia na matapeli.

Mwisho; Kumtongoza mwanamke mtandaoni na kuanzisha mahusiano nae ni jambo zuri. Ila kuanzisha mahusiano kwa njia hii, unaweza kutana na changamoto ya mtu kukuigizia maisha na kukudanganya kwenye vitu vingi sana. Kiufupi ni ngumu kutambua maisha halisi ya baadhi ya watu kupitia picha zao.

Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze Kila mala BONYEZA HAPA>>>

Leave a comment