Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Ukihitaji kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwenye simu, unaweza tumia kupitia njia mbili. Njia ya kwanza kabisa ni kutumia mtandao wa Facebook moja kwa moja katika tuvuti/website ya facebook. Njia ya pili ni kutumia Facebook kupitia app maalumu ambazo ni “Facebook lite” and “Facebook ya kawaida”.
Njia nzuri na rahisi ya kutumia mtandao wa Facebook ni njia ya app. App rasmi za Facebook zipo mbili, unaweza tumia app ya kawaida ya Facebook au ukatumia app ya Facebook lite ila kikubwa ni utambue tofauti ya app hizi. App hizi zinautofauti na hapa chini tumeweka tofauti chache kati ya Facebook lite na Facebook ya kawaida.

Tofauti kati ya Facebook Lite na Facebook ya kawaida kwenye simu yako

Matangazo mengi

Mtu unapotumia mtandao wa Facebook kupitia app ya Facebook lite hua unaoneshwa matangazo machache kuliko akitumia Facebook ya kawaida.
Unapotumia mtandao wa Facebook huwa kuna matangazo ambayo hujitokeza. Matangazo haya huioneshwa na kampuni ya Meta kwa kila mtu anaetumia mtandao wa Facebook Bure. Kuna watu hua wanalipia pesa Facebook ili kuyaondoa matangazo haya kwenye akaunti zao.

Kutumia data sana


Katika mtandao wa Facebook, Kuna vitu vingi sana ambayo mtu unaweza tumia bando lako kuvifurahia. Lakini unapaswa kufahamu huwa unapotumia app ya Facebook lite bando lako litatumika kidogo ukilinganisha na ukitumia Facebook ya kawaida.
App ya Facebook lite imeundwa kutumia data kidogo na inafanya vizuri hata kama upo kwenye mazingira ambayo mtandao unasumbua.

Kuchukua nafasi kubwa kwenye simu


Ukiingiza Facebook ya kawaida pamoja na Facebook lite kwenye simu yako kisha ukaangalia nafasi zilizochukua kwenye simu yako, utagundua Facebook ya kawaida imechukua nafasi kubwa sana kwenye simu yako kuliko Facebook lite.
Facebook lite ni app ndogo isiochukua nafasi kubwa sana kwenye Storage ya simu yako.

Ubora wa picha na video


Facebook lite ni app inayoonesha ubora wa chini wa picha ukilinganisha na app ya Facebook ya kawaida. Ukihitaji kuona ubora katika video na picha katika mtandao wa Facebook, tumia Facebook ya kawaida na sio Facebook lite. Facebook lite inawezapunguza ubora wa picha au video unapoziingiza au unapozitoa mtandaoni.

Katika video na picha za 360°

Kama ni mpenzi wa video na picha za 360° unatakiwa kufahamu huwa huwezi angalia video na picha za 360° ukiwa unatumia Facebook lite. Video na picha za 360° zinapatikana katika mtandao wa Facebook lakini unahitaji kuwa na app ya Facebook ya kawaida ili kuangalia kwenye kifaa chako.

Ni vema kufahamu tofauti ya app ya Facebook lite na Facebook ya kawaida ili uweza chagua unahitaji kutumia ipi, kwanini na wakati gani. Endelea kuwa karibu zaidi na The bestgalaxy.

Leave a comment