Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya Tendo (Wapenzi)

Kama ni mtu ambae upo katika mahusiano ya mapenzi na mmefikia hatua ya kutaka kucheza mchezo wa mapenzi, inaweza kuwa ni jambo zuri.
Mwanaume ikiwa umefika umri ambao unaruhurusu kufanya mchezo huu na mwanamke pia amefika umri, mnaweza kufanya mapenzi/tendo.
Lakini jambo hili linaweza kuwa zuri zaidi na salama kwenu kama mambo ambayo tunayaeleza hapa yatazingatiwa.

Mambo ya kuzingatia unapotaka kufanya tendo (mwanaume/mwanamke)

Usafi wa mwili

Usafi ni muhimu kuzingatia pale unapotaka kucheza mchezo wa mapenzi. Ikiwa wewe ni mwanaume au mwanamke, usafi unatakiwa kuuweka mbele maana uchafu unaweza mtoa mwenza wako raha ya mchezo. Hakikisha mdomo wako uko vizuri na hizo sehemu za mchezo husika siko safi pia. Epuka kuweka mdomoni vitu vyenye harufu mbaya na utumie vitu vinavyoleta harufu nzuri ili usimkere mwenza wako.

Kutumia kinga

Ikiwa mahusiano yenu yamewapeleka kucheza mchezo lakini hamjajuana vizuri, ni vema kuzingatia matumizi ya Kinga kwenye mchezo huo. Kinga ni muhimu maana huzuia mimba zisizotarajia na pia maambukizi ya baadhi ya magonjwa ikiwemo virusi vya Ukimwi. Ngono zembe inaweza kumpa mwenza wako au kukupatia wewe athari bila kujali wewe ni mwanaume au mwanamke. Ndio maana mtu anashauriwa kutumia mpira wa Kondom ambao ni Kinga unapokutana kimwili na mtu usiemjua kiundani.

Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>

Kuchukua tahadhari ya matukio mabaya

Kama mazingira ambayo mmekubaliana kucheza mchezo huu ni mageni kwako, ni vema ukachukua tahadhari. Hakikisha unakua makini ili vitu vyako visiibiwe, kuwa makini katika vitu unavyoweka mdomani ili usipewe dawa, kuwa makini pia usije kurekodiwa video na watu wabaya. Usiache kuzingatia jambo hili kama hata huyo mwenza wako hamjajuana vizuri maana baadhi ya watu huwa na nia mbaya tofauti na mapenzi.

Elewa mipaka yako na kuheshimu

Watu hucheza mchezo wa mapenzi na kila mtu huwa na mipaka yake katika mchezo huu. Sasa ni vema ukaelewa na wewe mipaka yako ni ipi na kuisimamia pale utakapokua ukicheza mchezo bila kumtoa mchezoni mwenza wako. Pia Kama mwenza wako atakua na mipaka, jiweke tayari kuiheshimu mipaka hiyo bila kutoka mchezoni. Na Kama mtavunja mipaka yenu basi ile kwa makubaliano.

Kuondoa woga wa kupita kiasi


Woga ukipita kiasi katika mchezo wa mapenzi, unaweza ushindwe hata kucheza mchezo vizuri. Baadhi ya wanaume wamekua wakishindwa kusimama uanaume wao kutokana na kuogopa. Ni vema kuondoa woga na kujiamini ukiwa Kama mwanaume au mwanamke ili ucheze katika nafasi yako vizuri na kumfurahisha mwenza wako.

Mambo hayo machache na yanaweza kuwa marahisi kuyapuuza, lakini ni mambo muhimu kuzingatia unapotaka kukutana kimchezo na mwenza wako hata ikiwa ni mara ya kwanza.

Leave a comment