Uangaliaji wa video online kupitia app kama Youtube,Tiktok na Instagram unaweza kua ni moja ya vitu ambayo hupelekea bando la internet kutumika sana kwenye simu. Kiufupi kama mtu anapenda kuangalia video sana mtandaoni basi hata matamizi yake ya data yanaweza kuwa ni makubwa na kupelekea bondo kuisha haraka. Hii inweza kuwa kawaida au ikawa tatizo kwa baadhi ya watu.
Hapa The bestgalaxy tunaendea kuangalia mambo machache ambayo mtu anaweza fanya kuangalia video Youtube bila kutumia bando sana. Kama unataka kujua mambo yaha hebu chukua muda wako kusomaa hapa chini.
Fanya haya kuangalia video Youtube bila kutumia bando sana
Washa Data saving mode
Youtube imejali matumizi ya data ya watumiaji wa app ya Youtube kwa kuweka kipendele kinachopunguza matumiza ya Data. Kuna kipegele ambaacho ukikiwasha katika app ya youtube, unakua unatumia bando lako la internet kidogo. Kipengelea hii kinaitwa Data saving mode na ukikiwasha huwa kinapunguza na kuzima baadhi ya vipengele vingine vya app ya Youtube vinavyotumia Data. Ni jambo zuri kutumia njia hii kuoa data lakini video hua zinaonekana hazina ubora. Kuwasha Data saving mode nenda katika app alafu gusa Profile yako kisha bonyeza alama ya settings iliojuu kulia alafu chagua “Data saving”. Baada ya hapo, washa sehemu ya juu ilioandikwa “Data saving mode”.
Chagua video fupi
Youtube inavideo fupi na ndefu. Kati ya video fupi na video ndefu katika kutumia data tunaweza sema uangaliaji wa video ndefu unaweza kufanya utumie data zaidi endapo video hizo zitakua na ubora wa picha sawa. Hivyo kama unahitaji kuangalia video Youtube bila kutumia bando sana unaweza angalia video fupi badala ya kuangalia video ndefu. Na hatakama utamaliza bado lako kwa uangalia video fupi utakua umeangalia video nyingi.
Zima Autoplay
“Autoplay” ni kipengele ambacho hufaya video ziwe zinaendelea kujiplay Moja baada ya nyingine mfulilizo pale zinapoisha. Kipengele hiki ni kizuri lakini ubaya wake ni kwamba ukijisahau unaweza kuta video nyingi sana zimejiplay na kumaliza bado lako la internet. Kama unahitaji kuzima kipengele hiki, nenda kwenye app yako ya Youtube kisha ingia kwenye Profile alafu gusa alama ya Settings na uchague “Autoplay”. Baada ya kufanya hivyo, zima Autoplay kwa kugusa kitue kilicho upende wa kulia.
Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy na usiache kutembelea mara kwa mara The Bestgalaxy ili kusoma vitu vingine.