Kuwa na mahusiano ya mbali ni jambo la kawaida kipindi hiki. Kuna mambo mengi katika maisha yanaweza fanya ukaanzisha mahusiano na mtu aliembali na wewe au ukaenda mbali na mtu ulie na mahusiano nae. Umbali katika mahusiano unaweza sababisha mahusiano kuwa katika hali ya kuvunjika kwa urahisi endapo hakutakua na mambo ambayo husaidia kutunza mahusiano. Unataka kujua mambo haya ni mambo gani? Sawa, hebu soma hapa chini.
Mambo ambayo hutunza mahusiano ya mbali (Mwanaume na Mwanamke)
Mawasiliano ni muhimu.
Mawasiliano ni jambo muhuimu lisilotakiwa kukosekana kwenye mahusiano ya mbali. Mawasiliano huwaunganisha wapenzi hata mukiwa mbali. Ni vema kufanya mawasiliano mara kwa mara na mtu ulienae kwenye mahusiano ili kulinda mahusiano yenu. Jisukume kumjulia hali mapenzi wako na kuzungumzane karibu kila siku mpaka mufikie ile hali ya kuhisi muko pamoja japo mupo mbali.
Uaminifu na uvumilivu
Katika mahusiano ya mbali, kupoteza uaminifu na uvumilivu ni rahisi sana. Uaminifu na uvumilivu ukipotea kwenye mahusiano ya mbali unaweza pelekea mahusiano kuvunjika. Ni vema kila mtu kwenye mahusiano hayo ya mbali akawa mvumilivu na kuonesha uaminifu kwa kuwa muaminifu kwa mwenzake. Mara nyingi mtu ukishaanza kutokua muaminifu kwa mwenzako aliembali, utaanza kubadili tabia zako kwake bila wewe kujijua. Hii inaweza pelekea mpenzi wako wa mbali kuanza kutokukuamini, kuumia na kushindwa kuvumilia au kukusaliti.
Kuongea kuhusu mambo yajayo na mipango ya mbele bila kujali umbali.
Unapokua unawasiliama na mtu ulienae kwenye mahusiano na mnaongelea kuhusu mambo yajayo au mipango ya mbele mnajenga picha ya Future ya mahusiano yenu pamoja na kwamba muko mbali. Ongeanae kuhusu kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, mwaka ujao na maisha yenu ya mbele kiujumla. Weka nae mipango, ongelea matukio yanu yanayokuja, wekeaneni ahadi ndogo na kubwa mtazo mtazokua mkiishi kuzitimiza, Ulizaneni kususu vitu mtavyo fanya kesho au mwisho wa wiki.
SMS nzuri kwa Mpenzi aliembali BONYEZA HAPA>>>
Kuonesha kuwa unampenda, unamjali na unatamani muwe karibu.
Muoneshe kuwa unampenda kwa kumwambia vitu vizuri, kumfanyia vitu vizuri vitakavyoonesha unamjali hata kama upo mbali. Kama amekwambia hayuko vizuri, usipuuze kisa muko mbali. Jaribu kuwa msaada kwake kwa njia itakayowezekana. Jali maneno yake na hisia zake pia alafu usisahau kuonesha kuwa unatamani muepamoja. Mwambie vitu vizuri unavyotamani toka kwake ukiwa huko mbali, muoneshe kua yeye ndie alieuteka moyo wako huko uliko na utamani awekaribu yako hata sasaivi.
Ni hayo tu tumekuandalia katika mengi unayoweza Fanya kutunza mahusiano ya mbali. Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usinchukie kutembelea Kila mara.
