Fortnite ni game lililotolewa na Epic Games katika mwaka 2017. Epic games ni kampuni inayojihusisha na Games na imetengeneza magemu mengi tu, ikiwemo hili game linaloitwa Fortnite. Tangu game hili limetoka mpaka sasa kuna mamilioni ya watu wanalicheza na baadhi ya watu wanaotumia simu za Android ni miongoni mwa watu hao.
Hapa chini The bestgalaxy tunatoa maelezo juu ya jinsi ya kulicheza gemu kwenye simu za Android online bila kudownload. Game la Fortnite halipatikani katika Playstore hii ni baada ya kuondolewa kwa kutofuata sheria za Google Play store. Liliondolewa mwisho wa mwaka 2020 na game nyingi zikikiondelewa katika Playstore huwa zinakufa lakini Fortnite ni game ambalo lipo hai mpaka leo na unaweza cheza kwenye simu yako ya Android kwa kudownload nje ya Playstore na hata kujeza bila kudownlod pia.
Magemu ya mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>
Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)
Kucheza gemu hili kwenye simu bila kulidownload ni rahisi tu japo utakitaji kuwa na internet yenye kasi, VPN pamoja na Accounti ya Microsoft. Kama hauna akaunti ya microsoft usihofu maana unaweza tengeneza katika ya safari ya kulicheza gemu hili. Fuata hatua zifuatazo kucheza game la fortnite online kwenye simu bila kudownload.
- Unganisha VPN na iwe kwenye server ya USA
- Tumia web browser yako kuingia katika Xbox.com/play
- Bonyeza kiduara cha upande wa kulia juu ya ukurasa wa kwanza wa Xbox.com/play
- Bonyeza batani ya kijani ilioandikwa “SIGN IN” alafu jaza taharifa za akaunti ya Microsoft. Kama hauna akaunti utabonyeza neno “Create One” utakaloliona baada ya bonyeza hiyo batani ya kijani.
- Baada ya kuweka sawa akaunti ya Microsoft utarudishwa kwenye ukurasa wa Xbox
- Utatakiwa kutumia kisehemu ya tafuta cha ukurasa huo kutafuta game la “fortnite” alafu kuliona utalichagua na kubonyeza “Play” ili kuanza kulicheza.

Unapocheza gemu hili, hakikisha internet yako iko vizuri maana ikiwa iko vibaya unaweza kutofurahia kucheza gemu la fortnite kwa njia hii. Njia hii ya kucheza gemu huwa inaitwa “Cloud gaming” na huduma ya” Xbox cloud gaming” ndio inayotumika maana inaruhusu kucheza gemu hili bure.
Kama wewe ni mtu uliekua USA na upo kwenye sehemu ambayo game hili halikupi nafasi ya kucheza basi hizo hatua juu ukizifuata utaweza kucheza gemu lako pendwa ukiwa nje ya USA.
One thought on “Jinsi ya kucheza game la Fortnite online kwenye simu (bila kudownload)”