Moja ya app zinazotupa uwezo wa kufanya miamala ya kifedha katika viganja vyetu ni app ya Mpesa. App hii ni kwaajili ya watumiaji wa Vodacom. Moja ya faida za kutumia app ya Mpesa kwa mtumiaji wa Vodacom ni kwamba hata laini voda ikiwa haipo hewani au imepotea, unakua umebaki na uwezo wa kufanya miamala kwenye app hiyo kwa kutumia internet ambayo haihusiani na laini yako ya voda.
Kuna baadhi ya watu wamekua wakiuliza juu ya kubook ndege za usafiri kwenye app ya Mpesa na hapa tunaenda kuangalia kuhusu hilo. Kama na wewe unahitaji kujua juu ya hili basi hapa unaweza pata mwanga.
Kubook ndege kwa app ya MPesa
Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?
Ndio, inawezekana. Precision Air na Vodacom waliungana na kukuletea uwezo wa kubook ndege kwenye simu yako kupitia app ya Mpesa. Kwa sasa app ya Mpesa inavipengele vingi ikiwemo kipengele cha kubook ndege za usafiri. Precision Air wamekiri kuwa huduma ya kubook ndege kwa app ya Mpesa ni huduma rahisi na haraka kwa watumiaji. Na pia moja ya kitu kizuri kuhusu kubook ndege kupitia app ya Mpesa ni kwamba unapata punguzo la asilimia 20 ambayo inaokoa karibu robo ya pesa yako. Kwaiyo tunaweza sema pia hii ni njia ya kupata tiketi za ndege kwa bei rahisi.
Kipengele cha kubook ndege kwenye app ya MPesa
Ukifungua app ya Mpesa unaweza kiona kipengele cha kubook ndege maeneo ya chini kikiwa kimeandikwa “Book Flights”. Kama umeangalia chini na haujakiona, mbonyeza sehemu ilioandikwa “Services” alafu ukisha fanya hivyo utapelekwa kwenye orodha ya huduma na utaona kipengele kinachoitwa Book Flights kwenye orodha hiyo. Ukifungua kipengele hicho utakutana na ukurasa huu chini kwaajili ya kutafuta na kubook ndege itakayofanikisha safari yako.

Asante kwa muda wako, Endelea kuwa karibu na The bestgalaxy na usisahau kutembelea kila mara kupata vitu vipya.
One thought on “Unaweza book ndege kwa app ya MPesa?”