Kuitwa Mume au mke haimaanishi hauitaji kumwambia mwenza wako unampenda au maneno mazuri ya upendo na mahaba.Watu wengi huisha ingia kwenye hatua ya kuitana mume au mke huwa wanasahau kuambiana maneno mazuri kiasi kwamba wanaweza kuyumbishwa kwenye mahusiano kwa kuanguka kimapenzi na mtu wa nje kisa anawaambia maneno mazuri na kuwasifia.
Kumwambia mke au mume wako maneno ya upendo ni jambo linaoweza mpa furaha na kuona unamjali haijalshi unatumia sms au unaongea moja kwa moja. Kama unataka kumtumia mke au mume wako sms za mahaba,hapa chini kuna orodha ya sms za mahaba kwa mume au mke ambazo unaweza tumia bure kabisa. Chagua zinazoendana na hali yako ya mahusiano ndio utumie.
Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>
sms za mahaba kwa mume au mke
Umeuweza moyo wangu mpaka nahisi umeniloga. Unaupa raha moyo wangu nikikukosa pembeni yangu napata homa. Pezi lako ni tamu na kila siku linazidi kunoga. Kwako nimefika vya wengine siwezi onja.
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu na kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi. Ukweli ni kwamba nikipata salamu yako huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana wangu.
Kuishi na wewe ni raha sana. Penzi lako ni zawadi niliopewa na mungu katika maisha maana linanifanya nione thamani ya kuishi dear. Nitakupenda milele bila kujutia.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika tendo BONYEZA HAPA>>>
Umenifanya nijione wa thamani toka pale uliponichagua kuwa wako maishani. Kwenye milima na mabonde umepambana mpaka sasa umekuwa na mimi. Asante kwa upendo huu honey, nitakupenda milele maishani.
Wewe ndie mfalme wangu, Mwanaume ninaekupenda kwenye dunia hii, Mtu ninaejivunia kuwa nae maishani na natamani popote alipo ajue kuwa pamoja na yote tunayopitia kwenye maisha, bado ameteka hisia zangu.
Acha leo nikwambie ukweli. Thamani ya penzi unalonipa ni kubwa kwangu na siwezi fananisha na chochote kwenye hii dunia. Namshukuru mungu kwa kunikutanisha mpenzi mwema unaejali hisia za moyo wangu, Nakupenda sana mpenzi, usichoke kunipenda.
Wewe ndie malaika wangu, Fundi wa raha zangu, Msaidizi niliepewa na mungu, Mwanamke mzuri ninaempenda kwenye ulimwengu mpaka nikaamua kumchagua yeye tu maishani mwangu na sasa natamani ajue kuwa sijawahi jutia kuwa nae maishani, upendo wake unanipa furaha isio na kifani.
Penzi letu haliwezi kuvutia kuila mtu hapa duniani. Natamani uzibe sikio la kusiliza wengine na unisikilize mimi tu. Ninaposema nakupenda nasema toka moyoni. Usisikilize ya watu mpenzi mimi nakupenda wewe tu hapa duniani.
