Kumwambia mpenzi wako nakupenda na kuchezanae mchezo inaweza kuwa ni jambo zuri lakini tambua kuwa bado unaweza onekana sio romanic. Kuwa romantic kumekusanya mambo mengi sana katika mahusiano. Kiufupi kuwa romantic ni kuonyesha mapenzi kwa mpenzi wako, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Hapa The Bestgalaxy tunafungua ubongo kwa kuelezea mambo machache ya kufanya ili kuwa romantic kwa mpenzi.
SMS za kumbembeleza mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako (Mwanaume au mwanamke)
Mwambie maneno matamu na yakuvutia
Kama uko pamoja nae mnaongea au unazungumza nae kupitia simu, hakikisha unamwambia maneno matamu na yakuvutia. Ongea na mpenzi wako kwa hali ya utulivu alafu mwambie maneno ya upendo toka moyoni yatakayo ugusa moyo wake na kumfanya ajue jinsi gani unampenda. Funguka mwambie moyo wako unahisi vipi juu yake au msifu kwa maneo matamu.
Mzawadie zawadi zitakazo mfurahisha
Mpe zawadi ambazo unahisi atazipenda. Zawadi sio lazima iwekubwa au sio lazima iwe pesa. Unaweza mzawadia mpenzi wako vitu vidogo sana na akafurahi mpaka ndani ya moyo wake. Unaweza mzawadia mpenzi wako hata pipi ya kijiti tu na akafurahi ila inategemeana na namna ulivyomzawadia au muko katika hali gani. Mbali ya vitu kama pipi unaweza mzawadia vitu vingine unavyoona anapenda au anahitaji ila hajakwambia.
Mpe muda wako muwe pamoja
Ni wazi kuwa kama unampenda mwanamke, unatamani akupe muda wa kuwa nea na hivyo hivyo hata mwanamke akimpenda mwanaume anatamani apate muda wa kuwa na mpenzi wake. Kutumia muda wako kuwa na mwenzako ni jambo linaloweza kufanya uwe romantic. Unaweza kutumia muda na mpenzi wako mukiwa mnaogea, mnacheza michezo ya upendo, kutembea, kuangalia vitu, kusikiliza au kusoma vitu.
Mtu akikublock WhatsApp Fanya hivi kuchati nae BONYEZA HAPA>>>
Mshawishi mwili
Kumbusu mpenzi wako, Kumshika mikono na kumkumbatia au kumgusa kwa ujumla ni mambo muhimu sana katika mahusiano maana ni vitu ambavyo vinaweza kukufanya uonekane romantic kwa mpenzi wako. Mchokoze kimwili mpezi wako na kama atakua na mahitaji ya kimwili ni vema ukaheshimu hisia zake. Siku hizi unaweza mchokoza hata kwenye simu kwakuongelea vitu vitakavyo msisimua kidogo.
Msikilize, thamini mawazo yake na tatua migogoro kwa upendo na amani
Msikilizea anachokwambia na uoneshe kuyathamini mawazo yake. Usipuuze mawazo yake anayoyasema maana atakuona humueshimu au kumjali. Kama kuna mgogoro umejitokeza kati yenu usiwe mwepesi wa kumjia juu kumfokea au kumtukana. Tafuta njia ya amani na upendo ya kutatua mgogoro huo. Sehemu ya kuomba msamaha muombe msamaha, Sehemu ya kubembeleza mbembeleze na sehemu ya kumsamehe msamehe.
Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani BONYEZA HAPA>>>
Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia zake. Pia majukumu au kazi isiwe sababu ya kushindwa kuonyesha mapenzi kwa umpendae, kumuonesha kuwa unamthamini na kumjali kwa kusema na kufanya matendo yanayogusa hisia. Ukishindwa kufanya hivyo mpenzi wako anaweza kuona sio romantic na wengine wanaweza wakakuacha kabisa maana hawafurahii mahusianio.
