Unataka kumuumiza mwanaume anae kutesa unampenda? Soma hapa

Kuna mwanaume ambae uponae kwenye mahusiano na unampenda lakini anakutesa? Unataka kufanya kitu kitakacho muumiza? Ni kitu gani unahisi ukikifanya kitamuumiza? Mh sawa ila kabla haujafanya maamuzi yoyote, hapa The bestgalaxy tunakujuza vitu vichache kuhusu hili.

Ni mara nyingi watu huangukia kwenye mahusiano ambayo huanza kwa kuwapa furaha lakini baadae hubadilika na kupoteza furaha kutokana na wenza wao kubadilika na kuanza kutojali hisia zao.Hali hii katika mahusiano inaweza kubadilika na kuwa nzuri au inaweza kuendelea kuwa mbaya zaidi na kupelekea kuvunjika kwa mahusiano kabisa.

Unapokua kwenye mahusiano alafu mwenza wako akabadilika ghafla na kuanza kukutesa au kutojali hisia zako ni vema ukajaribu kwanza njia mbali mbali kubaini nini tatizo na kurekebisha mahusiano yenu. Jaribu kuvumilia huku ukiongea na mpenzi kwa uwazi kabisa nakumuuliza  nini shida na mutafanya nini ili muwe sawa.

Uvumilivu ni jambo zuri sana pale mahusiano yanapoyumba ila kama mahusiano yanayumba na kugeuka mateso yasioisha mtu anaweza shindwa kuvumilia na kuanza kutafuta njia za kumuumiza anaemuumiza na hata kuondoka kwenye mahusiano kabisa. Kumuumiza mtu anaekuumiza kwenye mahusiano ni jambo baya sana maana linaweza pelekea ukajiumiza mwenyewe. Mfano; kuna dada moja alikua akiteswa kimapenzi na mwanaume wake. Akaamua kumuumiza mwanaume wake kwa kujiingiza kwenye mapenzi na rafiki wa mwanaume wake. Baade alipewa mimba na huyo rafiki alafu akapata na magonjwa pia kisha akatelekezwa. Unafikili uamuzi wa huyo dada ulimuumiza nani?

Ukiwa kama mwanamke, kuliko kufanya maamuzi yatakayo kuathiri hata wewe ni unaweza ukafanya yafuatayo.

Mambo muhimu kufanya kwa mpenzi mwenye hasira au ukorofI BONYEZA HAPA>>>

Mambo unayoweza fanya badala ya kufanya maamuzi mabaya

Jipende kuliko alivyokuzoea.

Kuna muda unaweza mzingatia sana mtu anaekutesa kiasi kwamba unasahau hata kujipenda. Unasahau thamani ulionayo na kujiweka hovyo hovyo. Ukiwa kwenye hali hii ni vema kuikumbuka thamani yako na kuanza kujipenda. Jipende bila hata kuambiwa unapendwa alafu jijali kwenye kila kitu. Vaa vizuri, pendeza, uwe msafi na ujiamini katika uwanamke wako ila usiwe na kiburi au dharau. Tambua kwamba wewe ni wa thamani na hata ukiambiwa “Sikupendi” bado thamani yako iko pale pale.

Usiingie kwenye mahusiano mengine kwa msukumo wa kuumiza mtu.

Ukiwa kwenye mahusiano ambayo mwenza wako anakutesa, kuna muda unaweza waza kutafuta mpenzi mwingine wa haraka haraka ili tu kumuumiza mweza wako. Wazo hili ni wazo baya sana maana linaweza kukufanya usiwe makini katika kuingia kwenye mahusiano. Jambo hili linaweza pelekea uingie kwenye mahusiano yatakayokupa shida na hata kukuacha katika hali mbaya zaidi.  

Usioneshe tena kuwa unaumizwa na mambo yake.

Kama kuna vitu mweza wako huwa anafanya kwa dharau ili kukuumiza na umejaribu kila mbinu kumzuia au kumwambia aache lakini anaendelea kufanya, acha kuonesha kuwa unaumia alafu kuwa kimya. Pengine anahitaji kukuumiza ndio maana anaendelea kufanya. Acha kumuonesha kuwa unaumia ili ajue amekuumiza mpaka umechoka. Kama atakua ni mtu anaejari, ataanza kuwaza mabadiliko yako.

Kubaliana hali halisi na ujipumzishe.

Ikiwa umevumilia na kujaribu kila njia ya kuokoa mahusiano yako lakini imeshindikana, kubaliana na hali halisi. Usilazimishe sana huwa kwenye mahusiano ambayo yanahatalisha mpaka maisha yako. Jaribu kurekebisha na ikishindikana kabisa, futa machozi alafu jipumzishe kwenye mahusiano hayo. Usifanye maamuzi yoyote mabaya.

Leave a comment