Kuna muda ukiwa kwenye mahusiano, unaweza tamani kumwambia maneneo ya mahaba moto moto mpenzi/mme/mchumba wako kwa njia ya ujumbe. Hili ni jambo hufanyiana wapenzi hasa mukiwa na upendo wa kweli kati yenu alafu munatumia sana simu kuwasiliana. Watu wengi wanapopokea jumbe au sms za mahaba toka kwa wawapendao, hufurahi.
Kama unataka kumtumia mpenzi wako sms za mapenzi motomoto basi hapa The bestgalaxy tunakupa sms za mapenzi motomoto ambazo unaweza mtumia mpenzi wako bila kuumiza kichwa sana. Kama utaona ni nzuri na zinaendana na mahusiano yako ya mapenzi, uaweza zitumia.
Maneno ambayo hautakiwi kusema kwa mwenza wako BONYEZA HAPA>>>
Sms za mapenzi motomoto (Mwanaume na Mwanamke)
- Siku hizi nanenepa kutokana na matunda unayo nipatia. Kila nikila nazidi kukung’ang’ania. Nafikiri wewe ndie mungu alinishushia maana umenipatia dear.
- Napenda kugusa ngozi yako laini kila nikiwa karibu yako. Kila ninapoigusa nahisi raha na msisimko. Hakika umeumbwa vizuri wewe mtoto, hahaha.
- Natamani unikumbatie nipate joto hapa nilipo. Natamani vitu vingi toka kwako japo siwezi sema. Nimekukumbuka sana mpaka nahisi siwezi hema.
- Natamani kusikia sauti yako mpenzi wangu. Unasauti nzuri inayougusa moyo wangu na kuulipua kwa furaha. Natamani tuishi pamoja ili niwe naisikia kila mara. Wewe ni tulizo la moyo wangu nakupenda sana.
- Natamani niwe na wewe kila siku,kila saa na kila dakika. Penzi lako moto naliitaji mpaka mwisho wa maisha. Nilikua naona mapenzi mabaya ila wewe kunakitu umenifundisha. Nakupenda zaidi ya sana.
- Ningerudi nyuma na kupewa nafasi ya kuchagua tena mtu ninaempenda, anaenifanya niwe na furaha na kunipa penzi linalo gusa moyo wangu bado ningekuchagua wewe. Nakupenda sana mpenzi wangu.
- Kukupata wewe kunanifanya nijione mwenye bahati sana katika dunia. Sijui sana kuhusu moyo wako ila tambua moyo wangu umeishazama katika penzi mpaka naogopa. Umeishaniteka sijiwezi mpenzi.
- Kuna watu niliwakaribisha kwenye maisha yangu wakanifanya nione mapenzi mabaya. Penzi lako nimefanya nione mapenzi matamu na sitamani niamshwe kwenye hii ndoto. Nakupenda sana.
- Nimeacha vitu vingi sana kwaajili yako na siwezi jutia maana unanipa furaha mpenzi wangu. Atuwezi kuwa sawa kila siku ila tambua nazidi kukupenda kila siku. Wewe ndie nimekuchagua moyoni na ndie daktari unaeweza tibu maradhi yangu. Wewe ni mtu wa thamani maishani mwangu.
- Penzi lako tamu, haliishi hamu. Upendo wangu kwako ni moto usiozima. Moyo wangu unalidunda jina lako na kila mara natamani kuwa karibu yako. Sijawahi penda kama hivi.
Mambo ya kushangaza usioyajua kuhusu Wanawake na Wanaume BONYEZA HAPA>>>
