Karibu The bestgalaxy na asante sana kwa kuwa hapa muda huu. Katika ukurasa huu tumekuandalia maelezo ya kukufungua ubongo juu ya jinsi ya kumiliki simu janja/smartphone bila kuwa na pesa nyingi. Maelezo haya yamelenga watu ambao hawatumii smartphone/simu janja mpaka sasa wakiamini hawawezi miliki simu hizi za kisasa kwasababu hawana pesa nyingi.
Ukweli ni kwamba usipokua unatumia simu janja kipindi hiki, unakuwa unapitwa na mambo mengi sana ambayo ungeyapata kiganjani kwako. Mfano mzuri ni kutumia app ya Whatsapp; kuna baadhi ya watu katika kazi zao wanashindwa kutuma au kutumiwa video,picha na vitu vingine kwasababu tu hawatumii app ya Whatsapp na sio kwamba hawapendi bali ni simu zao haziwezi.
Kuendelea kutumia hizo simu ndogo ni jambo zuri lakini kuanza kutumia simu janja kunaweza kuwa jambo zuri zaidi hasa ukijua matumizi mazuri na chanya kwako. Kama unataka kuanza kutumia simu janja lakini unauwezo mdogo sana kipesa unaweza fanya yafuatayo kupata simu janja kwa huo huo uwezo ulionao.
Jinsi ya kumiliki simu janja/smartphone bila kuwa na pesa nyingi.
Pata simu za mkopo na anza kulipa kidogo kidogo.
Moja kati ya vitu ambavyo watu hufanya sasaivi ni kuchukua simu za mikopo. Kuna makampuni huwa yanajihusisha na kutoa simu janja za mikopo. Unatakiwa kuwa na kiwango kidogo sana cha pesa ambacho utawapa alafu watakupa simu. Kiasi hicho cha pesa kinafahamika kama “kianzio” na kinaweza kuwa hata chini ya elufu 80 kwa baadhi ya simu(Ukubwa wa kianzio huwa kinategemeana na Thamani ya simu unayokopa). Baada ya kupewa hiyo simu utaanza kuitumia kama kawaida ila utatakiwa kuwa unalipia kiasi kidogo sana cha pesa kila siku mpaka utakapo maliza deni lako. Kiasi cha kulipa kila siku mara nyingi huwa kinakua ni chini ya Tsh 2000. Usipolipia simu hizi hua inajifunga na kukukumbusha kulipia ili uendelee kuitumia. Simu za mikopo ni nzuri sana kama hauna pesa nyingi za kununua simu ila unauhakika wa kupata pesa ndogo ya kulipia kila siku.
Nunua simu za ofa toka kwenye mitandao ya simu.
Mitandao ya simu kama vile Vodacom au Tigo huwa inakua na simu ambazo mtu unaweza zinunua kwa bei rahisi sana ukilinganisha na kuzinunua simu hizo kwenye maduka ya kawaida. Mara nyingi huwa mitandao hii inawaambia wateja wake kuwa watembelee katika maduka yao ili wajipatie simu za ofa. Ukienda katika maduka hayo utapata simu mpya za bei rahisi ambazo huwa zinakua mpaka chini ya 100000. Baada ya kununua simu hizo unaweza pewa bando la internet la kutumia mwaka mzima na pia huwa wanahitaji utumie mtandao wao kama mtando mkuu kwenye simu hizo. Hii ni njia nzuri ya kupata simu kwa bei rahisi hasa kama haupendi kuwa na deni.
Chukua simu zilizo tumika na mtu mwingine.
Muda huu kuna watu wanaziuza simu zao kwasababu mbali mbali na wamekosa wateja. Kuna watu wanauza simu laki 1 na waliinunua laki 3. Kuna watu wamezichoka simu zao wapotayari kuziuza hata chini ya laki. Unaweza pata simu nzuri tu toka kwa watu wanaoziuza simu zao ila utakiwa kuwa makini sana na simu hizi maana zinaweza kukupeleka pabaya. Ni vema ukikutana na mtu anaeuza simu ukamuuliza kwanini anauza, ametumia kwa muda gani inatatizo gani na kufuata taratibu zitakazo kuokoa pindi simu hiyo itakapokua imehuswa na tukio baya.
Ukitaka kupata simu inayouzwa mtaani kwako, tangaza kwa watu kuwa unahitaji simu ili hao watu wakisikia mtu anauzwa simu, wamlete muuzaji kwako. Kama hautaki kununua simu za mtaani kwako, unaweza tumia app kama Jiji au app ya Kupatana ila umakini unahitajika sana.