Ni kawaida sana kuona wapenzi wanaopendana kukutana na sababu mbalimbali zinazopelekea wapenzi hao kuwa mbali. Sababu hizi zinaweza kuwa ni kazi, masomo na mambo mengine katika maisha. Wapenzi ambao wako mbali au wanaoishi mbali ni vema wakazingatia sana mawasiliano na kuonyeshana upendo katika mawasiliano.
Hapa The Bestgalaxy leo tunakupa orodha ya jumbe fupi za mapenzi ya mbali zinazoweza kutumika katika kuwasiliana. Kama mahusiano yapo kwenye hali hii basi unaweza tumia jumbe hizi:
Jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
sms za mapenzi ya mbali
1. Umbali wowote kati yetu hauwezi kuuzima upendo wangu kwako Mpenzi. Kila siku nakuwaza na nazidi kukupenda tu huku natamani sana uwekaribu yangu.
2. Kukaa mbali na wewe ni kazi ngumu sana mpenzi wangu. Kuna muda natamani nije huko uliko niwe na wewe ila nikikumbuka kuwa kuna siku tutaonana, napata amani kidogo, Nakupenda sana.

3. Hata kama tuko mbali kimwili, moyo wangu daima uko nawe huko uliko. Nakupenda sana.
4. Napenda tunanyowasiliana, unanifanya nijisikie karibu nawe japo tuko mbali. Kichwa changu na moyoni mwangu bado upo wewe mpaka tutakapokutana tena.
5. Kuna malaika wa upendo nimenitokea na kuniambia kuwa penzi letu linapendeza. Umbali hauwezi kututenganisha mpenzi wangu, tuendele kuwa pamoja milele.
6. Usiruhusu shetani atumie mwanya wa sisi kuwa mbal,i kuua penzi letu. Penzi letu ni kubwa kuliko umbali wetu. Siwezi kukuona au kukugusa huko uliko ila tambua moyo wangu wote upo kwako.
Jinsi ya kutunza mahusiano ya Mbali BONYEZA HAPA>>>
7. Sikuizi nakosa joto lako tamu unalonipa pindi nikigusa mwili wako. Lakini bado nakupenda kwa nguvu zote. Jina lako limeandikwa ndani ya moyo wangu na haliwezi futika milele. Unaeweza fanya niumie au niendelee kufurahi ni wewe.
8. Moyo angu hulipuka kwa furaha kila tunapowasiliana. Hii ni kwasababu nakupenda na siku zinavyozidi kwenda, nazidi kukupenda leo kulio jana. Sipati picha nitakavyokua tukikutana.
9. Moyo wangu uko nawe, hata kama mwili wangu uko mbali na wewe. Umbali hauwezi yumbisha penzi langu kwako. Nikishindwa kuvuilia nipo tayari kukufuata na sio kukuacha kipenzi changu.
10. Jukumu la kulinda penzi letu ni langu mimi na wewe mpenzi. Tunapokua mbali au karibu ni vema tukakumbuka jukumu letu mpenzi. Tusije ruhusu walioharibu mapenzi yao waalibu na yetu. Nakupenda sana.

Jumbe au sms kama hizi zinaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wenu wa mbali na kumfanya mpenzi wako ajisikie kuthaminiwa na kupendwa. Pia ni vema kukumbuka kuwa mawasiliano ya mara kwa mara na jitihada za kukutana zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye uhusiano wa mbali.