Kumekuwa na mahusiano mengi ambayo huanzishwa lakini hayafiki mbali kama lilivyo lengo kuu la mahusiano yao. Hali hii inafanya wanawake wengi wawe na wasiwasi katika mahusiano. Wamekua wakifikilia “Je, atanifanya niwewake wa maisha?” Lakini wanasahau kujiweka tayari kwaajili ya kuwa wanawake wa maisha.
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza mfanya mwanaume akuweke moyoni na akufikilie kuwa wewe ni wake wa maishani. Hebu tumia muda wako kuvisoma hapa chini.
Mazoezi ya mwili ambayo husaidia katika Mapenzi BONYEZA HAPA>>>
Mambo humfanya mwanaume akupende sana na kukuchagua maishani
Tabasamu.
Kama unahitaji mwanaume avutiwe na wewe basi tambua kitu muhimu kufanya unapokuanae ni kutabasamu na kucheka. Usionyeshe uso usio na urafiki. Kuwa kama mtu anayependeza, mwenye urafiki, na mchangamfu. Ukijitahidi kuwa mtu mwenye furaha kuliko maugomvi. Onensha sura ya tabasamu kuliko makasiliko. Mapenzi yenu yanaweza kuwa na furaha pia na hakuna mwanaume asiependa mapenzi yenye furaha.
Whatsapp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa BONYEZA HAPA>>>
Kuwa mcheshi.
Wanaume kwa ujumla wanapenda wasichana wenye ucheshi ambao wanaweza kuwafanya wajisikie vizuri. Kuna muda mwambie hadithi za kufurahisha na usiogope kucheka. Kumbuka usizidi kupita kiasi hadi uonekane kama mchekeshaji. Ni vizuri kuwa na mwenzi ambaye anafurahisha, lakini ni watu wachache sana wanamawazo ya kuishi na mchekeshaji.
Toa kuliko kuchukua.
Ili kuongeza nafasi zako za kukupenda lazima utoe kuliko kuchukua. Mwanaume anaweza kutofautisha kwa urahisi kati ya msichana ambaye anataka kitu kutoka kwake na yule anayemjali.
Nadhani unajua kuna wasichana wengi ambao wanafuata pesa na wameweka mbele pesa kuliko mahusiano. Wanaume wengi wanao wafuata wanawake wa mtindo huu huwa hawana mpango nao wa maisha maana huona kama wananunua upendo hivi… Jitofautishe na wauzaji na aone unavutiwa naye kwa upendo wake na sio pesa yake au kitu kingine chochote. Yani hata akitanguliza gari mbele usishoboke nalo sana kuliko kumpenda yeye maana baadae anaweza anza kulisifu gari kwa kukukamata wewe na mbaya zaidi inaweza kuwa ni wanawake wengi walinaswa na gari hilo hivyo, haunajipya.
Mpenafasi ya kufanya kazi, Mshauri na kumtia Moyo.
Katika maisha Mwanaume maranyingi huzungukwa na vitu vinavyomkatisha tamaa na kumuumiza lakini anatakiwa ajikaze tu kwasababu ni “Mwanaume”. Hii inaweza kuwa kazini, kwenye familia na maeneo mengine. Endapo mwanaume anaejielewa atapata mwanamke ambae anamsikiliza mambo yake magumu, anamshauri, anamtia moyo na kumsukuma kufanya maamuzi mazuri na maendeleo hata kwenye mambo madogo kwenye maisha, hawezi kumuacha mwanamke huyo aondoke maishani mwake. Kuna familia huwa zinainuka na kuwa na mafanikio kwasababu ya jambo hili, hasa zikiwa na mambo ya kidini ndani yake.
Kama muko kwenye mahusiano na mwanaume na anaonekana kuwa busy sana na kazi mpaka anafikia kuwa mbali na wewe, Usimfikilie tofauti moja kwa moja na kuanza vurugu. Mruhusu mwanaume afanye kazi kidogo ili kufanya maendeleo kisha vumilia pindi anapokua mbali na wewe ila usijisahau kumuonesha upendo sana.
Hili ni jambo ambalo linaweza kuongeza sana nafasi zako za kushinda upendo wake. Wanawake wegi wanakata tamaa na kumuacha mwanaume wanapoona yupo busy Sana na maisha… huzani kuwa hawana nafasi tena lakini jua kuwa wakati huo ndio wakati mzuri wa wewe kuongeza upendo wake kwako.
Jinsi ya kuwa romantic kwa mpenzi wako BONYEZA HAPA>>>
Muoneshe kuwa bado yupo moyoni wako, muoneshe kuwa unajua anachokifanya na ukipata muda muulize maswali au kumshauri, muoneshe kuwa bado unamjali hii itamfanya akuweke katika fikila zake za kimaisha. Usijekosa maisha mazuri anayokupambania kwa kukata tamaa.
Lakini unapo mruhusu afanye kazi mbali na wewe hakikisha unafanya vitu vya upendo ambavyo vitamfanya aanze waza kukuweka karibu yake au kuja karibu yako(kama atakua na uwezo huo). Ukipata nafasi pia mtembelee au fanya mautundu akutembele.
#Muvumilie anaejali upendo na uvulilivu wako tu, Wanaume wengine hukimbia mazima.
Usimmiliki sana kuliko kumuonesha upendo.
Wanawake wengi hufanya makosa ya kumiliki sana mwanaume na wakati hata hawamuoneshi upendo. Unaweza kujaribu kumlinda sana asiende kwa wanawake wengine ili abaki kuwa na wewe pekee katika maisha yake lakini je anao wafuata wanamvuta kama jinsi unavyo fanya wewe?. Ni wazi kuwa wanamvuta kwa upendo na vitu vingine vizuri… hivyo na wewe kuwa mbunifu na kwenye kumuonesha upendo ambao utamvutia zaidi kisha mruhusu aamue kuchagua kinachomfaa. Ikiwa wewe ndiye wa kwake, hakika atakupenda.
”kwanini wanawake wazuri/warembo hawaolewi?” sababu zinaweza kuwa hizi BONYEZA HAPA>>>
Kuwa na maadili mema.
Maadili mazuri ni lazima katika kumshawishi mwanaume akupende zaidi na aweke moyo wote kwako maishani. Hakuna mtu anayetaka kujihusisha na mtu ambaye haeleweki,hasikii au hana nidhamu. Bila shaka kila mtu husita kumpa moyo mtu ambae hana maadili mazuri. Wanaume wanapenda wanawake ambao wana nidhamu. Hivyo basi muheshimu na pia uwevizuri nae ataona unafaa kuwa wake maishani. kuna mambo unawezasikia rafiki au mwanawake wa mitandaoni Eti “Ukinichiti nakuchiti” “Wanaume wote ni Mbwa” “Siwezi kuwa na mwanaume mwenye gari au pesa” “Siwezi olewa kwa sasa mimi ni mzuri” na mengine mengi kama hayo. Ukileta mambo hayo kwenye maisha yako unaweza angukia pua, ni vema kutula kuwa na maadili yatakayomkaribisha mtu kuwa na wewe maishani. Onesha heshima kwa Mwanaume hata wakikuita mshamba. Kuwa msafi, vaa vizuri na marafiki wastaarabu.
