Jinsi ya kujua mtu mwingine anaona sms na unavyofanya WhatsApp kisiri

Whatsapp ni mtandao mkubwa ulimwenguni ambao watu huutumia sana katika mawasiliano. Unaweza kuwa ni mtandao wako pendwa katika mawasilioano ndio maana upo hapa… Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy, utajifunza vingi kuhusu mtandao huu.

Whatsapp ni mtandao mzuri kuutuumia katika kuwatumia watu Picha, Video, Audio au ujumbe wa maneno lakini unapofanya hivyo tambua kuwa kunajinsi ambavyo mtu mwingine anaweza kuona vitu vyote hivyo kwenye simu au kifaa chake bila wewe kutambua(kisiri). Kuna njia ambazo hata mtu asiebobea sana katika maswala ya Teknolojia anaweza tumia kuona sms au vitu unavyofanya kwenye Whatsapp. Lakini jambo hili lisikutishe maana hapa chini tunakwenda kukujuza jinsi ya kuangalia kama upo salama na jinsi ya kujilinda pia… Kwaiyo ondoa hofu na endelea kutumia Whatsapp yako kama kawaida.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Jinsi ya kujua mtu mwingine anaona sms na vitu unavyofanya WhatsApp kisiri

Whatsapp kwa sasa inakuruhusu mtumiaji wake kuunganisha akaunti yako moja ya Whatsapp kwenye kifaa zaidi ya kimoja. Unaweza fannya akaunti yako moja ya WhatsApp iwe inatumika kwenye simu mbili mpaka 4 na namba ikawa hiyo hiyo moja. Mtu mingine anaweza kuitumia hii kunganisha akauti yako kwenye simu yake au kifaa chake na kuanza kukuchunguza unachofanya bila wewe kujua. Na mtu akitumia ataweza kusoma sms zako, kujibu, kuona na kuchua audio,video na vitu vingine unavyotuma na kutumiwa bila wewe kujua.

Ukitaka kujua kama akaunti yako ya Whatsapp imeunganishwa fanya yafuatayo:

  1. Fungua Whatsapp yako na uguse Vidoti Vitatu
  2. Ukifanya hivyo, Chagua “Linked divices”
  3. Baada ya kufanya hivyo utatupwa kwenye ukurasa ambao ukikuta kuna kifaa chochote kiorodheshwa basi jua whatsapp yako sio salama. Na kama hamna kifaa basi yawezekana upo salama. Unaweza angalia picha hapa chinikuelewa zaidi.

Endapo utakuta akaunti yako ya Whatsapp sio salama(hacked) unaweza gusa kifaa kilicho orodheshwa kwenye kwenye ukurasa huo alafu ukagusa vidoti vitatu itakavyoonekana juu kulia kisha utachagua “Remove device”.

Ili kuhakikisha kuwa WhatsApp yako iko salama kila mara, hakikisha unafanya kuangalia kama akaunti yako ya WhatsApp imeunganishwa mara kwa mara hasa baada ya kumruhusu mtu mwingine aishike simu yako bila uangalizi wako.

Mtu akikublock WhatsApp Fanya hivi kuchati nae BONYEZA HAPA>>>

2 thoughts on “Jinsi ya kujua mtu mwingine anaona sms na unavyofanya WhatsApp kisiri”

Leave a comment