Maneno na maswali ya kurefusha maongezi na kumfurahisha mpenzi wako

Katika mahusiano wapenzi mnaweza ongea au kuwasiliana mpaka ikafika wakati mkakosa cha kuzungunzia, hasa kama hakuna mmoja kati yenu mwenye uwezo wa kuendesha mazungumzo. Ukiwa kwenye hali hii, unaweza ingizia maneno na vimaswali vilivyopo hapa chini kurefusha mazungumzo yenu, kumchekesha na hata kukusaidia kumjua vizuri mpenzi wako. Unaweza kuyatumia kama sms, au kuyaongea unapokua nae karibu au kwenye simu. Lakini unapotumia maneno na maswali haya hakikisha hamupo kwenye hali ambayo itamfanya mpenzi wako aone kero. Endelea kuwa karibu na The Bestgalaxy.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Maneno na maswali ya kurefusha maongezi na mpenzi wako

  1. Kuna watu walikua wanamsifia dada flani hivi kuwa anamacho mazuri, nilivyomwangalia yule dada nikajiuliza “Mh hivi wanamjua mpenzi wangu hawa? hahaha” Unamacho mazuri sana alafu nayapenda.
  2. Hivi hilo kovu ulifanya nini?, au ulikua cha utundu utotoni?
  3. Kama kuna zawadi ambayo ulipanga kumpa mtu atakae kupenda kwa dhati maishani mwako nipe tu maana nakupenda sana mpenzi, sitamani utoke maishani mwangu unanipa furaha mwenzio. Stamani niamke kwenye hii ndoto.
  4. Kwa mfano umeshida Milioni 80 sasa hivi, utanipa shingapi au utafanyia nini?
  5. Kukupenda ndio kitu ninachoweza kukifanya bila kuchoka duniani mpenzi wangu. Sijui niwe nakuita jina gani ili usije sahau kuwa nakupenda na usinitende…
  6. Ulivyo kuwa mdogo ulitaka ukiwa mkubwa uwe nani?
  7. Hebu fumba macho tuone… Hahaha Unamacho mazuri… ivi unajua kwamba una macho mazuri hivyo?
  8. Kwaiyo umelala peke yako? huogopi?
  9. Wiki ijayo nikumbushe nikwambie kitu… Ntakwambia kitu kizuri
  10. Kitu gani unapenda utimize kabla siku zako za kuishi duniani hazijaisha?
  11. Bebi, ivi nikikwambia utaje vitu vitano tu unavyo penda duniani utataja vitu gani?
  12. Unapenda mbwa au paka?
  13. Ivi katika maisha yako unaogopa nini?
  14. Ulifikiria nini mara ya kwanza nulipokwambia nakupenda?
  15. Niambie vitu vitatu tu ambavyo hauvipendi?
  16. Ivi umenipendea nini? au unapenda nini toka kwangu mpenzi?
  17. Ninavyokugusa huwa najiskia vizuri sana ivi wewe unahisi vipi?
  18. Unafanya nini sasa hivi?
  19. Upo na nani hapo kipenzi?
  20. Natamani nije hapo japo kukubusu tu lips zako nzuri hizo
  21. Ukichukia unapenda kufanya nini ili kutuliza hasira zako?
  22. Alafu usiku nilikuota
  23. Ivi umeishawahi poteza hela? ilikua kiasi gani?
  24. Niambie maneno matatu mazuri toka moyoni mwako
  25. Unapenda kuangalia filamu? unapenda filamu gani?
  26. Hahaha… nitakwambia kesho… au nipe zawadi nikwambie leo
  27. kwenye familia yenu wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?
  28. Ivi bebi Unapendelea zaidi kula chakula gani?
  29. Ugali kwa kiluga chenu munauitaje?
  30. Ukipewa nafasi ya kutembelea nchi tatu duniani ambazo hauja wahi tembelea, utachaguza zipi?

Leave a comment