Magemu mazuri ya mabasi kucheza kwa simu za Android

Magemu ya mabasi yamekua ni kati ya magemu pendwa sana kipindi hiki. Magemu haya yapo mengi sana na watu huyacheza kupitia simu, pc na baadhi ya vifaa vingine kama hivyo vinavyo tuwezesha kucheza magemu. Katika makala hii tunazungumzia magemu mazuri ya mabasi lakini tutajikita katika upande wa simu za Android hivyo kama wewe ni mtumiaji wa simu yoyote ya Android, unapenda na kutaka magemu mazuri ya mabasi, hii ni kwaajili yako.

Kutokana na wingi wa magemu ya mabasi kwa simu za Android, inaweza kuwa ngumu kwa mtu kujaribu kila gemu ili kujua lipi ni zuri na lipi ni baya kwake ingawa unaweza fanya hivyo pia. Hapa sisi tunakupa orodha ya magemu macheche ya mabasi ambayo ni mazuri unayoweza kuyacheza katika simu yako na yanachezwa na watu wengi duniani. nafikili hii inaweza kukusaidia katika utafutaji wa gemu zuri kwako.

WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

Magemu ya mabasi za kucheza kwenye simu za Android(5)

1. Bus simulator 2023

Katika magemu ya Android mazuri ya nayohusiana na uendeshaji wa mabasi, kunage hili linaitwa “Bus simulator 2023”.Bus simulator 2023 ni gemu la mabasi lililotoewa na Ovidiu Pop kwa simu za Android pamoja na iOS. Lilinakutupa katika ulimwengu ambao unakua ni deleva wa mabasi na kuna modes nyingi unaweza kuwa unafurahia humu ndani. Unaweza kucheza na marafiki aua watu wengine online na pia kwenye upande wa muonekano uko poa. Asilimia kubwa ya watu waliolicheza gemu hili,wamelipenda kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo muonekano.

2. Bus simulator indonesia

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa The bestgalaxy unawezakuwa umegundua kuwa gemu la Bus Simulator Indonesia tumeliongelea zaidi ya hapa. Hii ni kwasababu nigemu zuri sana na usioweza kuyaacha unapozungumzia magemu ya simu ya kuendesha mabasi. kwasasa gemu la Bus simulator indonesia imeishaingizwa kwenye simu na watu zaidi ya milioni 100 kutoka sehemu mbalimbali za dunuia. Mazingira na mabasi ya katika gemu hili ya yanaendana na mabasi na maingira halisi ya huko Indonesia. Muonekano wa gemu hili ni mzuri na pia uzuri mwingine wa gemu hili ni hutohitaji kutumia data/internet katika kulicheza ingawa ukihitaji kucheza na watu au marafiki, utahitaji kuwa na muunganiko wa internet(data).

3. Coach Bus Simulator

Hili ni gemu la mabasi ambalo mpaka sasa watu zaidi ya milioni 10 wamelipakua katika vifaa vyao vya Android OS. Ndani ya gemu hili mchezaji unaendesha mbasi ya abilia ya masafa kuwatoa sehem moja kwanda nyingine. Na ukiwa kama dereva wa mbasi unakumbana na changamoto mbalimbali katika kazi yako unapokua barabaradi. Linamuonekano mzuri. Ovidiu Pop ndio waliotoa gemu hili na linapatikana bure kabisa kwa watu wote wanaohitaji kulicheza katika Android. Unaweza kulipakua kupitia Playstore na ukaanza kufurahia kulicheza kila siku bila kutumia data(Ni gemu la Offline).

4. Bus simulator ultimate

Katika mwaka 2019 “Zuuks Games” walitoa gemu la Bus Simulator Ultimate na toka hapo mpaka sasa kuna mamilioni ya watu wamepakua gemu hili na wanaendelea kulicheza. Zuuks Games walisema gemu lao la bus simhlator limekua ni miongoni mwa magemu ya mabasi yaliopakuliwa na watu wengi… limeshafikisha zaidi ya watu milioni 200. idadi hiyo ya watu inajumuisha watu kutoka US,UK,Canada na sehemu nyingine yingine nyingi za dunia, ikiwemo Tanzania. Unaweza kulidowmload au kulipakua gemu hili bure ila kulicheza utahitaji kutumia data(internet).

5. Public Transport Simulator C

Gemu jingine zuri la mabasi kwa upande wa Android ni hili linaitwa Public Transport Simulator C. 2019 ndio mwaka SkisoSoft walilitoa na tokalitolewe mpaka sasa limechezwa na zaidi ya watu milioni 50. Kutokaa na uzuri wake asilimia kubwa ya watu wanaolidownload na kulicheza wanalipenda na hii imeionesha kupita reviews ambazo zimekua zikitolewa na wachezaji wa game hili katika Playstore. Pamoja na kwamba gemu hili limetolewa mwaka 2019 lakini bado linaendelea kuboreshwa na hupata updates kila baada ya muda flani… Lakini jambo hili halifanywi kwenye gemu hili tu, hufanywa kwenye mgemu mengine. Kiufupi ni kwamba magemu yanaboreshwa Kila siku na Unaweza ona Gemu ni baya Leo lakini baada ya mwaka likawa limeboreshwa na kuwa zuri.

Mbali na magemu haya unafikili ni gemu gani lingine zuri kwa upande wako? Huu ni mwisho wa orodha yetu,, usiache kuwa kalibu nasi…

Leave a comment