Asubuhi ni mwanzo wa siku na kuianza siku vizuri kunaweza kuwa ni pamoja na kupokea sms ya maneno ya upendo toka kwa watu tunaowapenda. Kumpa maneno mazuri ya upendo mpenzi wako wa moyoni anaekupenda kunaweza kufanya aifurahie siku nzima na pengine kufanya aendele kukuamini kwamba unamjali, upo yupo kichwani mwako na unamuwaza huko uliko. Hivyo kama unataka kufanya jambo hili, tambua kuwa hizo ni kati ya faida zake katika mahusiano. Na kama unahitaji sms za maneno mazuri za asubuhi zitakazo mgusa roho mpenzi wako, unaweza ukoa muda kwa kuangalia sms fupi ziliopo hapa chini zitakazo endana na hali ya penzi lenu.
Mambo ya kuepuka katika mahusiano BONYEZA HAPA>>>
SMS za asubuhi njema kwa umpendae
Asubuhi njema… Natamani siku ya leo tungeamka kitanda kimoja na wewe. Tena sikufichi, huku niliko nakosa vitu vingi sana kwasababu niko mbali na wewe mpenzi wangu… Ila nikikumbuka kuwa unanipenda na pia nakupenda, moyo wangu unatulia kidogo na kusubilia siku tutakayoonana ingawa naona kama nachelewa kukutana na wewe malaika wangu, nakupenda sana.
Upendo ni zawadi ya pekee sana mungu aliyoiweka ndani ya mioyo yetu bure na mimi nimeitumia vema sasa zawadi hii kwa kukupenda wewe. Nakupenda sana na sijawahi jutia kukupenda mpenzi wangu. Asubuhi njema wangu.
Sms za kumfanya mpenzi wako afurahi BONYEZA HAPA>>>
Kuna mtu mmoja mzuri, anaakili sana, mkarimu na nampenda saaaana, yupo anaisoma sms hii niliomtumia pekeyake asubuhi hii. Ameuteka moyo wangu na sihitaji kuunasua maana anaupa raha kwa penzi lake, Asubuhi njema kwake.
Natumai ulikuwa na usingizi mzuri sana. Tafadhali amka sasa kwa sababu asubuhi yangu haiwezikamilika kujua hali yako wewe. Habari ya asubuhi mpenzi!
kila siku huwa nawaza kukusu wewe na mapenzi yetu kiujumla… nimegungua najifunza vitu vingi sana toka kwako, pia upendo wako unaboresha maisha yangu na kunifanya niishi kwa furaha sana. Asante kwa kuwa mimi, nimekuweka moyoni, nakupenda na nazidi kukupenda kila siku mpenzi wangu, Asubui njema kwako.

Natumai umelala kama malkia. Sasa tafadhali amka kama nyota na utawale ulimwengu wangu kwa siku ya leo tena. Habari za asubuhi!
Katika penzi letu kunamuda tunagombana alafu tunapatana. Hii isije kukufanya uamini kuwa sikupendi. Kama jinsi jua linavyo chomoza asubuhi hii na kuleta mwanga palipo na giza ndivyo uwepowako unaleta furaha kwenye maisha yangu. Nakupenda sana na najivunia kuwa na wewe…. Nakutakia asubuhi njema wangu.
Tunapitia vitu vingi katika penzi letu lakini sijawahi jutia kukupenda wala kuwa na wewe kwenye penzi. Mimi huwa naamini mimi ni Mfalme na wewe ni Malkia katika safari ya maisha na penzi letu, naamini unanipenda na nakupenda sana. Nakutakia asubuhi njema na siku yenye furaha.
Jinsi ya kufanya mpenzi wako akuwaze kila mara BONYEZA HAPA>>>
Leo nimeamka nikiwa na mawazo yako tu akilini mwangu. Huwezi amini nilivyo kumiss hapa. Siezi kufurahia asubuhi hii nzuri bila wewe mpenzi wangu. Amka!
Najisikia kubarikiwa sana kila asubuhi ya maisha yangu ninapojua hali yako ni salama. Umeamka poa?
