Fanya haya baada ya kondomu kupasuka katika tendo

Mpira wa kondomu hutumika katika tendo la kujamiiana ili kuzuia mimba na vile vile hutumika kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. 

Katika utumiaji wa mipira ya kondomu kupasuka kwa kondomu hutokea mara nyingi Sana bila kutarajiwa. Mara nyingi kitendo hiki husababisha mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Hapa kuna hatua nne unazoshauriwa kuzifuata iwapo kondomu imepasuka:

1. Kuwa mtulivu na tafuta kondomu hiyo iliopasuka.



Mara nyengine kwa mwanamke vipande vya mpira huo wa kondomu vinaweza kuingia ndani ya mwili.

Ingiza vidole vyako ndani ya mwili, vishike na kuvitoa nje.

Mipira ama vipande vya kondomu vinavyosalia ndani ya mwili wa binadamu vinaweza kusababisha hasara hivyobasi ni muhimu kuangalia na kuhakikisha kuwa umetoa kondomu yote.

2. Tumia dawa za kuzuia kushika mimba iwapo hamjakubaliana kupata mtoto(Kwa mwanamke)



Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72 tu. Zinauzwa madukani yaani zinapatikana katika maduka ya dawa.

Iwapo huna mpango mbadala unaweza kutumia dawa za kupanga uzazi.



3. Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan HIV iwapo hujui hali ya mwenzako




Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliofanyika.

Pia unaweza kuchukua dawa aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP) katika kipindi cha saa 72.

PEP ni mchanganyiko wa dawa za kukabiliana dhidi ya virusi vya ukimwi ambazo zinakuzuiwa kutoambukizwa HIV iwapo mwenzako ni mwathiriwa.

Kumbuka kwamba kila ugonjwa wa zinaa una muda wake wakati unapoambukizwa na wakati utakapoonyesha unapopimwa.

Unashauriwa kufanyiwa vipimo zaidi vya vya magonjwa ya zinaa baada ya mwezi na baada ya miezi sita ili kujua hali yako.



4. Jiulize kuhusu kilichosababisha na usirudie kosa.





Wapenzi wengi huruka hatua hii bila kujua kuwa hayo ni makosa makubwa, kwa sababu utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndipo unaweza kujiweka vizuri katika mchezo mwingine. Hivyobasi jiulize kuhusu hilo.

Leave a comment