BANGE SIO CHAI..
Siku moja Nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi,Mjusi(lizard) akaja akampa “Hi” akajiunga na kumuomba puff.
Nyani akamuonya kuwa ile bangi ilikuwa ni kali sana,ni kipisi cha kutoka Milimani huko. Mjusi akapokea wakaanza kuvuta bangi kwa raha zao…baada ya muda mjusi akawa hoi kwa stimu akamuambia nyani “Duh nasikia koo langu limekauka acha niende mtoni nikanywe maji!”
Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na stimu nyingi akatumbukia mtoni. Bahati nzuri Mamba alikuwa pembeni, akawahi kumuokoa mjusi na kumtoa nje ya maji.
Baada ya kumuokoa, Mamba akamuuliza mjusi “Ina kuwaje bro mbona umetumbukia mtoni kipuuzi vile?” Mjusi akajibu “Nilikuwa na nyani tunavuta bangi nikasikia kiu ya ajabu nikajikuta kwenye maji bila kujua!” Mamba akasema “Aaah wacha niende huko kwa nyani nikamuone.”
Mamba kufika akamkuta nyani ndo anamalizia kipisi chake,kazidiwa hata macho ni tabu kufungua. Mamba akamuita “Oya” Nyani akafungua macho,kumuona Mamba akashtuka Et”Duh! Mshikaji kwani umekunywa maji yote mtoni! Mbona umerudi mkubwa hivyo!!”
SIPATI PICHA INGEKUAJE…
Jamaa yangu mmoja alikuja kunitembelea kule Mburahati Madoto. Sasa wakati namsindikiza tukafika kituo cha madoto mwisho
kusubiri daladala. Mara jamaa yangu akanyewa na kunguru kichwani. Jamaa akaangalia juu alivyogundua amenyewa akamuona
kungulu usawa wake, jamaa akaangua kicheko sana yaani. Mi nilikuwa naona yote yanayotokea nikamuuliza “sasa unacheka nini
ndugu yangu wakati umenyewa?” Jamaa akajibu “We acha tu, afadhali bata hawapai angani kama kunguru”
AMRI KUMI KWA WAPENDAO OFA
- Muheshimu anayekununulia
- Muamkie mtoa ofa kabla hujakaa kitini
- Uwe ndie mchekeshaji wa kikao, lakini usimkatishe mazungumzo anaetoa ofa
. Mtoa ofa akikutuma popote usikatae - Mtoa ofa akiupenda muziki fulani, we anza kucheza kwa bidii kabisa
- Usinywe kwa pupa, kunywa mafunda madogomadogo
- Mtoa ofa akitoa kichekesho cheka sana hata kama hakichekeshi