Unasumbuliwa na speed ndogo ya internet? Usiwe na wasi tena! Hapa The Bestgalaxy tunakufungua juu ya nini unachoweza kukifanya kufurahia internet nyenye kasi kwenye simu yako ya smartphone.
Moja ya vitu ambavyo huudhi katika katika matumizi ya internet ni speed/ kasi ndogo. Speed ndogo ya internet sio tu huudhi bali pia hupoteza muda wa mtu anaetumia internet kwasababu kitu ambacho alitaka kukifanya kwa dakika 1 kwenye internet kinaweza mchukua mpaka dakika 5 ikiwa speed ya internet itakua ni ndogo. Watu wengi wanao thamini muda huchukizwa na swala hili.
Lakini tukirudi kufikilia kahusu historia ya internet utagundua internet imebadilika Sana na huwezi fanananisha na kipindi cha nyuma. Hata internet ya sasa isumbue vipi kwenye speed lakini huwezi ilinganisha na zamani maana huko nyuma internet ilikua haina kasi kabisa kama ya sasa. Kudownload nyimbo Moja tu yenye Mb 5 ilikua inaweza kukuchukua mpaka saa 1. Kama ni mtumiaji wa muda mrefu wa internet unaweza kuwa unajua kuhusu hili.
Yafuatayo ni mambo ambavyo Unaweza fanya kuongeza speed ya internet kwenye simu yako (hayahusishi matumizi ya WiFi)
WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>
Namna ya kuongeza speed ya internet kwenye simu
1. Hakikisha unatumia laini ya 4G au 5G na Simu 4G au 5G
Kwasasa ukitaka kufurahia kasi nzuri ya internet basi inatakiwa iwe ni kuanzia kasi ya 4G. Ukitaka kufurahia kasi hii ya internet kwenye simu yako ya smartphone inatakiwa iwe na laini ya 4G na pia simu yako iwe ni ya 4G au 5G. Mbali na havyo pia ni vema “preferred network type” yako ikaiseti kwenye “Auto“. Kuiset preferred network type kwenye simu yako nenda kwenye “settings” ingia kwenye na uende katika “Network & internet” alafu ingia kwenye “SIM cards” kisha ingia kwenye “Mobile network“. Baada ya hapo gusa “Preferred network type” na uchague “Auto“.
2. Hamia kwenye mtandao wa simu wenye huduma ya internet yenye kasi.
Kuna muda mtu anaweza kuwa unakumbana na changamoto ya kasi ndogo ya internet katika matumizi ya internet kutokana na mtandao wa simu unaokupa huduma ya internet kutokua vizuri katika maeneo uliopo. Jaribu kufanya utafiti kwa watu uwalio kuzunguka ili kujua mtandao wanotumia kupata internet na speed yake ya internet iko vipi. Unaweza tu kuwaambia watu “Mimi ninatumia mtandao flani kupata huduma ya internet lakini naona Kama haupo vizuri Sana katika speed kwenye maeneo haya… Ivi ni mtandao gani nyinyi mnautumia na upo vizuri?”

Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>
Kama kutakua na mtandao wanao sema upo vizuri basi jaribu na uangalie kama utakua vizuri kwako pia. Unaweza pia wasiana na watu wanao husika na mtandao wako wa simu na kuwataalifu kuhusu Jambo unalopitia kwenye eneo lako ili warekebishe. Tena bahati nzuri ni kwamba sikuizi makampuni ya mitandao ya simu ina kurasa zake katika mitandao ya kijamii na Unaweza watumia ujumbe kule na wakakujibu.
3. Boost speed ya internet kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima.
Kama speed yako ya internet inasubua subua wakati unaitumia unaweza kuwa unaiboost kwa kuwasha “Flight mode” na kuizima. Flight mode huwakilishwa na kialama Cha “ndege ya usafiri” na hupatikana katika kisehemu Cha simu unachokifuata pindi unapo washa Data kwaajili ya kuanzia kutumia internet.
4. Tumia app zinaweza ongeza Speed ya internet.
Kuna baadhi ya app za VPN zinaweza ongeza speed ya internet. Hii inaweza onekana zaidi unapo download vitu au ku-stream vitu online ukiwa unatumia VPN. Lakini app za VPN zipo maalum kwaajili ya kuufanya muunganiko wako wa internet uwe salama na si kuongeza speed. Na pia sio kila unapotumia VPN utapata internet yenye kasi, VPN zinaweza pia kupunguza kasi kabisaa.
Mbali na app za VPN pia Kuna app zinazohusisha zaidi DNS zinaweza kuongeza kikasi Cha internet unapotumia. Mfano mzuri ni app iitwayo WARP… Unaweza ijaribu kwuingiza kwenye simu yako ya Android kwa lugusa hapa au iPhone kwa kugusa hapa