Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi

Kipindi cha mwisho wa mwaka ni kipindi kizuri sana cha wapenzi kutumia muda wao pamoja. Sasa kama unampenzi basi katika ukaribu wenu wa kipindi hiki unaweza kumtumia mpenzi wako ujumbe mzuri utakao mfurahisha na kujiona wa peke katika maisha yake. Hapa tume kuandalia jumbe nzuri unazoweza mtumia mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi. jumbe hizo ni zifuatazo;


~~~~Tulikutana, tukapambana ili tubaki pamoja, tukashinda na tulikua na nguvu katika changamoto zote tulizokabiliana nazo mpaka kufika hapa. Nafikili penzi letu litazidi kuwa imara zaidi. Nimependa kutumia Christmas hii kukukumbusha kuwa, nakupenda sana mpenzi wangu.~~~~

~~~~~~Penzi lako ni zawadi bora ambayo ninaweza kuifurahia zaidi! Krismasi njema, mpenzi!~~~~

~~~~Siku zinakwenda, masaa yana kwenda mimi bado nipo na wewe. Unaona naishi kwa furaha, naona kuishi ni raha lakini tambua sababubu kubwa ni wewe. Tafadhari usije sahau kuwa nakupenda na moyo wangu umetekwa na wewe.~~~~~~

~~~~~Krismasi inakuja mara moja kwa mwaka, lakini tafadhali jua kwamba ninakuenzi kila siku, bila kujali umbali kati yetu. Christmas njema mapenzi wangu.~~~~~

~~~~Nakutakia Christmas njema mme/mke wangu… Nakupenda Sana na ningependa popote ulipo utambue una nusu ya moyo wangu na nusu niliobakinayo yote inakupenda wewe.~~~~

~~~~Penzi letu ni changa bado lakini upendo wangu kwako upo zaidi ya unavyoweza kufikilika, nakupenda Sana na nafurahi kila nikikuona mbele ya macho yangu hakika umeteka hisia zangu. Nakutakia furaha msimu huu wa sikukuu na nitafurahi zaidi tukitumia wote siku ya Christmas.~~~

~~~~~Wewe ni ua zuuri lililoota katika bustani ya moyo wangu, tena ni ua pekee la thamani, linalonipa furaha katika maisha yangu. Nakupenda Sana na najivunia kuwa na wewe malaika wangu. Kuwa na furaha tele katika msimu huu wa sikukuu, kipenzi changu!~~~~~~

~~~~~Hakuna raha kama kupendwa na wewe na sijawahiona karaha kuwa na we. Kama moyo wangu ungekuwa wazi, ungejiona ukiwa peke yako na ukobusy kunipa furaha. Nakupenda Sana na nakutakia furaha katika msimu huu!~~~~~

~~~~Katika Christmas hii nitapenda niwe na furaha, na nikae na mtu ninaempenda na anipae furaha. Vyote hivyo vitakamilika endapo tutatumia siku hiyo pamoja maana utanipa furaha na vile vile nitakuwa na wewe nikupendae na unapae furaha. Mpenzi, tutakua wote si ndio?~~~~

~~~~~Wanasema furaha haiwezi kupimwa kwa maneno halisi, Ni kweli. Tambua kuwa Krismasi hii inatukumbusha kwamba upendo, furaha, na nia njema ndio vitu halisi vinavyoinua maisha yetu. Asante kwa furaha unayoniletea tangu nilipokutana na wewe, mpenzi wangu.~~~~~

One thought on “Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako katika kipindi cha Krismasi”

Leave a comment