Kuibiwa simu(Smartphone) ni Jambo ambalo karibia kila mtu hapendi limtoke lakini huwa linamtokea tu pasipo kutarajia. Ukiwa bado upo na simu yako unatakiwa kuandaa mazingira ya kuipata kirahisi pindi itakapoibiwa. Ili kuipata simu iliobiwa unatakiwa kuwa na taalifa ambazo zitatumika katika kufanikisha zoezi la kuitafuta simu yako. Taalifa hizo ni pamoja na namba za IMEI za simu.
Jinsi ya kufanya simu isiishe chaji haraka GUSA HAPA>>>
Kila simu huwa na namba zake za IMEI na endapo utaenda polisi ili wakusaidie kutafuta simu yako basi utahitajika kuwapa namba za IMEI za simu ilioibiwa ili kufanikisha upatikanaji wake. Hivyo ni muhimu kuwa na namba za IMEI za simu zetu ili tukipoteza tuzipate kirahisi.
Sasa unachotakiwa kufanya kabla simu yako haijaibiwa ni kwenda katika sehemu ya kupiga simu alafu piga namba *#06# Kisha zinakili katika karatasi namba(IMEI) utakazoletewa na utunze karatasi hilo kwenye vitu vya muhimu ili lisipotee kirahisi.

Kama utakuja kupapoteza simu yako, namba hizo zitatumika kuipata simu yako pindi utakapo peleka swala lako polisi. Pia kumbuka kutunza na lisiti ya ununuzi wa simu.
Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>
4 thoughts on “Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa”