Mpira wa miguu ni mchezo maarufu zaidi duniani. Hapa tutajadili kuhusu magemu ya mchezo huu maarufu.
Katika ulimwengu huu, mbali na kutazama mechi ya moja kwa moja za mpira wa miguu, kuna watu wengi wanaopenda kucheza magemu ya mpira au Kandanda. Kuna ambao wanapenda kucheza magemu kupitia vifaa vya kucheza magemu kama vile, Playstation . Na watu wengine hutumia simu kucheza magemu ya mpira wa miguu.
Unaweza pia kuwa mmoja wa watu wanaotumia simu kwenye michezo ya mpira wa miguu ndio maana uko hapa. Ikiwa wewe ni mmoja wao basi hapa ni sahemu nzuri kwako. Tunakupa orodha ya gemu 5 bora za Mpira unazoweza kucheza kwenye simu (Android)
Bila kupoteza muda wako, sasa twende moja kwa moja kwenye orodha ya magemu bora ya mpira au soka kwa simu ya Android.
Download na kuangalia movie zote bure kwenye simu GUSA HAPA>>
Magemu bora ya mpira kwa simu ya Android
1. FIFA Mobile.
FIFA Mobile ni mojawapo ya magemu bora ya Soka ya Android kwa mashabiki wa soka. Gemu hili limetolewa na EA. Huchezwa Kwa kutumia Data, yaani huitaji internet.
Katika gemu hili unaweza kujenga timu yako ya ndoto na kuanza safari ya soka. Na unaweza kuijenga kwa kusajili superstars unaopenda katika soka.
Linakuruhusu kucheza au kushindana na watu wengine mtandaoni.
Battle Of Agents: Gemu kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet GUSA HAPA>>>
2. eFootball.
Gemu hili hapo awali ulilitwa “PES” lakini sasa ni “eFootball“. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni moja ya watu ambao tayari umecheza magemu ya PES, basi hii pia ni PES lakini PES imebadilishwa jina kuwa eFootball.
Kwenye orodha hii ya mgemu bora ya mpira ya simu za Android, tunaongeza gemu hili kwasababu ni gemu nzuri. Muonekano kwenye gemu hili ni mzuri.
Ili kucheza gemu la eFootball kwenye simu ya Android unahitaji kutumia intaneti. Kwa maneno mengine tunaweza kusema gemu hili hutumika Data japo ni bure kupakua na kucheza.
Simu yako lazima iwe na zaidi ya 2G RAM, Android 7 na 3.3GB ya nafasi ili kuwa na gemu la eFootball bila matatizo. Pia ikiwa na CPU 1.5 GHz au zaidi itaifanya ifanye kazi vizuri zaidi.
3. Dream league Soccer.
Dream league Soccer (DLS) ni gemu lingine la mpira au soka linaliweza kucheza kwenye simu simu. Gemu hili lilitolewa na First Touch games limited. Katika gemu hili unaweza kuunda timu yako ya ndoto na kusaini wachezaji wako unaowakubali wa mpira wa miguu kwenye timu yako.
Internet huitajika ili kucheza gemu hili kwa sababu ni DSL ni gemu linalihitaji data kulicheza. Lakini kulipakua na kuicheza ni bure ingawa ukihitaji, unaweza kununua baadhi ya vitu ndani ya gemu kwa pesa halisi.
Fanya haya kabla simu yako haijaibiwa ili kuipata ikiibiwa GUSA HAPA>>>
4. Total Football.
Total Football ni gemu lililotolewa mwaka 2022 (Beta). Gemu hili huchezwa Kwa kutumia Data/internet japo ukiwa Haina data unaweza kunavitu unaweza kuvifanya kwenye gemu na vikakufurahisha. Studio Vega Private Limited ndio wamelitoa gemu hili.
Kwenye gemu hili unaweza kuunda timu yako, kusaini wanasoka mashuhuri kisha kuipeleka timu yako kileleni. Jumla ya mchezo wa Kandanda ni mzuri sana na ni bure kuucheza na Kupakua kwenye simu ya Android.

5. Pro League Soccer.
Ikiwa unataka gemu zuri la Android ambao haliwezi hata kuchukua nafasi kubwa ya simu, gemu hili ni kwa ajili yako. Pro League Soccer ni gemu la simu la mpira was miguu ambalo ni dogo kuliko tulioyataja juu. Unaweza kuona gemu hili ni tofauti na magemu kama vile FIFA au eFootball lakini inafurahisha sana kulicheza. Linakuruhusu kuandika majina ya wachezaji na hata kutengeneza Jezi unavyotaka.
Mojawapo ya jambo zuri ni kwamba, gemu la hili linaweza kuchezwa bila internet.
Hivi ndivyo tunamaliza orodha hii. Lakini kumbuka kuwa kuna zaidi ya magemu ma 5 bora ya mpira kwa simu za Android ingawa tume orodhesha magemu matano pekee.
Ikiwa unataka kujua zaidi kuhusu magemu ya simu na vitu vingine basi usisahau kutembelea tovuti hii kila siku. Daima tuko hapa kukufahamisha mambo mengi.
WhatsApp yako inatatizo? Jifunze jinsi ya kutatua hapa>>>>

3 thoughts on “Magemu ya Mpira ya kucheza kwenye simu”