Fanya mambo haya kuifanya simu ijae chaji haraka

Kama umekua ni mtu unaesumbuliwa na simu katika masuala ya chaji, hasa kwenye upande wa simu kuchelewa kujaa pale unapoichomeka chaji basi nakujuza ni vitu gani ambayo unaweza kufanya ili kuifanya simu yako ijae kwa muda mfupi sana.

Lakini kabla ya yote ningependa kukukumbusha kuwa endapo utakua na maswali kuhusu jambo lolote linalokutatiza kuhusu simu yako, hakikisha unawasiliana na sisi. Pia usiache kufuatilia Kila post mpya ili kujifunza maana vitu vingi zaidi vipo mbeleni.
Zifuatazo ni njia ambazo ukizifanya unaweza ifanya simu yako ijae chaji kwa haraka sana.

Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>


1. Zima simu wakati unaichaji

Kuizima simu wakati wa kuichaji kunaweza ifanya simu ijae haraka sana kuliko ikiwa imewashwa. Ni vema sana kuitumia njia hii wakati ambao unahitaji simu ijae haraka na pia hufanya betri kujaa kwa utumivu na hii huimarisha hata betri lako. Lakini tatizo la njia hii ni kwamba husababisha mtu usiwe hewani hivyo basi ni vema kuitumia pale unapokua unajua kutokuwa hewani kwako hakutokupunguzia chochote.

Jinsi ya kupata mkopo kwenye simu GUSA HAPA>>>>

2. Washa Airplane mode unapo ichaji

Airplane mode hupatikana sehemu ile ya juu inayoshushwa pindi tunapowasha Data. Huwakilishwa na alama ya ndege za usafiri. Ili kuiwasha utatakiwa kuishusha sehemu ya juu ya simu yako kisha gusa alama yake kama unavyogusa pindi unapowasha Data. Njia hii hufanya simu ijae haraka mno lakini tatizo ni hautaweza kupokea wala kupiga simu maana Airplane mode ikiwashwa huvifunga vitu hivyo.

3. Washa power saving mode

Hii inaweza kuwa ni app ambayo huzizima baadhi ya app ili kupunguza matumizi ya chaji. Hupatikana kwenye arodha ya app ulizonazo au katika sehemu ya juu ya simu (Mara nyingi huwakilishwa na alama ya betri ilioambatana na alama ya jumlisha). Uzuri wa kutumia njia hii ni kwamba, utaweza kupiga au kupokea simu bila tatizo huku simu yako ikiendelea kujaa kwa kasi. Lakini simu nyingi za kisasa haziruhusu kuwasha power saving mode wakati simu ikiendelea kuchaji. Sio tatizo, unaweza pakua power saving mode app itakayofanya kazi hii kutoka Playstore. Natumani unaelewa jinsi ya kufanya simu ijae chaji haraka. Endelea kuwa nasi kujifunza vitu vingi zaidi.

Magemu mazuri ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>

Leave a comment