Simu kuingia maji Ni moja ya mambo ambayo hutokea katika shughuli zetu za Kila siku. Jambo hili huogopesha sana maana husababisha mpaka baadhi ya simu kupata matazizo au kutowaka kabisa. Hatuwezi zuia simu zetu kuingia katika maji maana hutokea Kama ajali, lakini tunaweza zuia simu zibaki salama yaani zisiwe na matatizo yoyote baada ya kuingia kwenye maji.Kama simu yako imeingia maji na unahitaji iwesalama basi fanya mambo yafuatayo;
Jinsi ya kupata mkopo kwenye simu GUSA HAPA>>>>
1. Zima simu
Baada ya simu kuingia maji unatakiwa kuhakikisha aiendelei kuwaka. Izime bila kupoteza muda maana ikiendelea kuwaka maji yalioingia yatasababisha vitu vya ndani ya simu hiyo kuharibika.
2. Chomoa betri
Kama simu yako inachomoka betri hakikisha unachomoa betri na kuliweka pembeni ya simu ila kama simu yako si ya kuchomoka betri, Fanya kuichoma line au memory Kisha kimbia moja kwa moja kwa fundi ili aifungue na kutenganisha vitu ili ikauke Kwa uhakika.
Download na kuangalia movie zote bure kwenye simu GUSA HAPA>>>
3. Iachewazi katika sehemu kavu

Chomoa line ya simu,Memoy na ikiwezekana nenda kwa fundi aliopo karibu na wewe ili aifungue ibaki wazi na kukauka kirahisi. Baada ya kuiweka wazi unatakiwa kuiweka sehemu kavu kwa muda mrefu mpaka itakapokauka kabisa.
Zingatia: usijaribu kuiwasha simu kwa kuijaribu kabla ya kufuata hatua hizi!
Ukweli kuhusu mchele: Watu wengi huweka simu zao katika mchele wakiamini simu zao zitapona lakini kitu cha muhimu kukijua ni kwamba, mchele ni unaweza kukausha maji lakini Kuna uwekano wa asilimia 4 hadi 1 ya maji yalioingia kubaki ndani ya simu na kuleta matatizo ambayo yatakuja kuonekana mbeleni. hivyo kabala ya kuweka huko unatakiwa kufuata hatua hizi pia.
Mtu akiku “Block” WhatsApp unaweza fanya hivi kuchati nae GUSA HAPA>>>
Kama itakua si maji ila vimiminika vingine: kama simu itangia katika pombe,Maji ya chumvi na vimiminika vingine, utatakiwa kuzima na kutoa betri kisha Kifungua nakuisafisha au kuifuta na kitambaa maana usipofanya hivyo baadhi ya vimiminika vikikaukia ndani ya simu, huozesha baadhi ya vitu vilivyo ndani ya simu (ukishindwa ni bora upeleke kwa fundi).
Nyongeza: Kuna baadhi ya simu zimeundwa kutoathiliwa na maji kabisa(Water proof). Yani hata ikidumbukia kwenye maji huwa maji hayaingii ndani ya simu. Lakini pia kunasimu ambazo zimeundwa kuzuia maji Kwa muda flani au maji ya joto flani(water resistant) lakini hazuii Kwa asilimia 100%. Simu hizi unaweza zidumbukiza kwenye maji dakika Moja au mbili na kuzitoa bila tatizo. Mara nyingi masharti yake ni maji yasiwe joto na usizidishe muda.
Endelea kuwa nasi kujifunza vitu vingi zaidi.

3 thoughts on “Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini?”