Kama ni mpenzi wa muda wa kuangalia mpira wa miguu wa nje ya nchi, nadhani umeshawahi kosa kuangalia mechi ulioipania kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwa mbali na Tv. Teknolojia inazidi kukua kila siku na kuturahisishia mambo. Sasa unaweza angalia mechi Kali za mpira wa miguu kupitia simu yako mubashara(Live) ukiwa popote. hapa tutakujuza jinsi ya kuangalia mpira wa nje karibu mechi zote kwenye simu yako BURE.
Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini? GUSA HAPA>>>
Ikiwa unahitaji kuangalia mpira live kwenye simu yako, utahitajika kuwa na app maalumu kwaajili ya kuangalizia mpira. App hizi zipo nyingi sana katika playstore(Android) lakini mimi nakushauri uchukue app nyepesi na isiokula sana Mbs iitwayo Live Football Tv.
App ya Live Football Tv ni app ya kuangalia mpira live kwenye simu yako. Mpaka Sasa inatumiwa na zaidi ya watu Milioni ulimwenguni na wanaisifu kwa kuonesha mipira mingi bila matatizo. Mbali na kukuonesha mechi live(mubashara), huwa inakupa matokeo na video za matukio muhimu ya mechi zilizomalizika kwaiyo Kama haukua na bando la kutosha kuangalia mpira mzima, unaweza angalia video ya goli lilivyofungwa tu. Pia inakupa nafasi ya kuangalia vipindi vingine vya kimichezo bure toka Ptv sports.

App hii ya kuangalia mpira live haipatikani Playstore kwasasa ila unaweza kitafuta Google na kuipakua. Pia Unaweza ipakua kirahisi kwa kugusa hapa>>> INSTALL. Na baada ya kuipakua, hauitajiki kujisajili au kufanya Jambo lolote la kujiunga ili kuitumia. Ni kuifungua na kuinjoi…
Fahamu kuwa: App nyingi zinazowezesha kuangalia mpira bure huendelewa Playstore kutokana na Kuvunja sheria za Playstore. Ikiwa app nilioitaja nayo itaondelewa basi unaweza ipakua app nyingine nje ya Playstore Kwa kugusa HAPA>>>
Jinsi ya kuangalia mechi za Tanzania kwenye simu GUSA HAPA>>>
Je, ni Mbs ngapi zinahitajika kuangalia mpira mzima(Dk90) kwenye simu?
Hili ni swali ambalo wengi hujiuliza, wanapohitaji kuanza kuangalia mpira kupitia simu. Ukweli ni kwamba, kadri video inavyokua na muonekao mzuri ndivyo Mbs huwa zinalika nyingi. Itakua ni vizuri zaidi Kama hautakua na chini ya Mb900 ili kutokua na wasiwasi wa bando kuisha.
Magemu ya Mpira ya kucheza kwenye simu GUSA HAPA>>>
