
Kama wewe ni mpenda magemu na unatumia simu yako ya Android kucheza magemu basi hapa tumekuandalia orodha ya magemu machache ambayo unaweza ya cheza na ukafurahia zaidi muda wako wa kucheza magemu kwenye simu yako. Kama ndio kwa Mara ya kwanza unataka kujifunza au kuanza kucheza magemu ya Android basi ni vema ukaangalia magemu yalio katika orodha hii na ukaangalia linalo kufaa kisha ukalipakua.
Call of Duty mobile

Hili ni gemu zuri sana la kivita ambalo limetolewa na Activision. Gemu la Call of Duty mobile ni gemu lililochezwa na watu Wengi na Mpaka sasa linaendelea kuchezwa na mamilioni ya watu ulimwenguni. Kama unapenda magemu ya kivita basi gemu hili unaweza kulifulahia zaidi lakini unachotakiwa kujua nikwamba game hili ni la Online. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema gemu hili linahitaji internet ili kulicheza. Kitu kizuri kuhusu magemu hili ni kwamba unaweza kucheza na watu wengine na pia Kuna mode ningine za kucheza zinazoweza kufanya usichoke kulicheza. Ili kulipata kirahisi gusa HAPA
Jinsi ya kutengeneza Avatar kwenye Facebook (Katuni)
Bus Simulator Indonesia

Bus Simulator Indonesia ni moja ya magame ambayo huchezwa na watu wengi sana na mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 50 na wengi hulifahamu kwa jina lake la BUSSiD. Ni game lililotolewa mwaka 2017. Game hili ni la Online yaani ili kulicheza utahitajika kutumia data. Kama nimpenzi wa game za muundo huu basi hakikisha unapakua game hili maana ni game zuri sana.Kitu unachotakiwa kukifahamu ni kwamba mazingira na magari yalio katika game hili yanayofana na mazingira ya Indonesia ndiomana likawa na jina Indonesia.Linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja (Online). Linapatika playstore kwa MB zisizopungua 272. Unaweza kulipakua kirahisi kwa kugusa HAPA
Traffic Rider

Kama ni mtu unaependa magame mazuri na unavutiwa zaidi na game za pikipiki basi game la Traffic Rider ni game litakalokufurahisha zaidi.
Game hili mpaka Sasa limechezwa na watu zaidi ya Milioni 7 ulimwenguni na asilimia kubwa ya watu hao wamelipenda.
Linamuonekano mzuri, Sauti zenye uhalisia na majira yenye uhalisia maana kuna hadi mission za usiku. Kadr unavyoendesha kasi pikipiki na kuovertake magari ndivyo unavyojiongezea idadi ya Scores. Lina missions zaidi ya 70 na kuna zaidi ya pikipiki 20 tofauti tofauti.Traffic Rider ni game lipatikanalo Playstore na lina MB90 tu. Hukubali mpaka katika simu zenye RAM 1 bila shida yoyote. Kama utahitaji kulipata kirahisi game hili gusa HAPA
Jinsi ya kutengeneza Pesa kwa kucheza games mtandaoni BONYEZA HAPA>>>
Occupation 2.5

Ni gemu ambalo unalicheza ukiwa Kama mtu ambae upo kwenye mji uliochafuka na kila mtu naeishi katika mji huo anaishi kwa hofu kubwa kutokana na uwepo wa wafu wanaotembea yaani Zombies na baadhi ya viumbe vingine visivyo na urafiki na binadamu. Ni moja ya magame mazuri yanayopatikana kwa Mbs chache katika playstore. Lina nyumba zinaingilika na unawachezesha wahusika zaidi ya mmoja katika mji huo. Unaweza kulipata kirahisi game hili kwa kugusa HAPA
EA Sports UFC

Unapenda magemu ya kupigana? Kama Unapenda magemu ya kupigana basi gemu la EA Sports UFC ni game ambalo halitakiwi kukoswa kwenye simu yako. Gemu hili ni moja ya magemu mazuri sana ya kupigana. Lina muonekano mzuri mno ambao utakufanya ufurahie kulicheza. Linahusu kupigana kwa kutumia ngumi na mateke.
Ukiona dalili hizi Jua Account yako ya Facebook imedukuliwa na si salama GUSA HAPA>>>>
Limekusanya wapiganaji wengi maalufu duniani ambao utatakiwa kuwafungua kutokana na uchezaji wako. Gemu hili linaweza kuchezwa Offline na Online. Ukiwa unacheza Online unakua na uwezo wa kucheza na watu wengine toka sehemu mbalimbali za dunia na utatakiwa kupambana nao na kufanya wapoteze dira kwa vitasa(ngumi) na mateke ya mitindo mbalimbali ili uibuke mshindi. Unaweza lipata katika playstore kwa kugusa HAPA
Overkill 3

Hili ni gemu zuri sana la Action ambalo mpaka sasa limechezwa na watu zaidi ya milioni 5. Linamuonekano mzuri na watu wengi wanalipenda kutokana na muonekano wake unaofanana na Caver Fire. Gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia linaweza kuchezwa na watu zaidi ya mmoja kwa kutumia data (Online).Inashauriwa anaecheza gemu hili awe na miaka 16 na kuendelea.
Overkill 3 ni gemu lipatikanalo Playstore kwa kama MB 401 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Takashi Ninja Worriror: Shadow of last samurai

Hili ni moja ya magemu mazuri sana ambayo kwa sasa yako trend katika playstore. Gemu hili ni la kijapani na linamuhusu kijana Takashi ambae anaingia katika kulipa kisasi kutokana na watu wake kufanywa vibaya. Ukilipakua utaweza kulicheza muda wowote na bila kukugharimu chochote maana gemu hili huchezwa bila data (Offline) pia hupatikana kwa MB chache sana zisizopungua MB 87.
Unaweza kulipata kirahisi katika playstore kwa kugusa INSTALL
Modern Strike Online

Ni moja ya magemu bora ya kivita ambayo huchezwa Online tu. Limechezwa na watu wengi sana wasio pungua Milioni hamsini(50).Gemu hili ni moja ya magemu yanayofanana na gemu la Call of duty hivyo kama unapenda magemu ya jamii ya Call of duty, usiache kucheza game hili.
Katika game hili unaweza cheza na marafiki zako Online kwa kiunda timu ya kuwaangamiza maadui au mukashindana kuua maandui ili atakaewaua maadui wengi awemshindi.
Modern Strike Online ni gemu lipatikanalo Playstore kwa MB zisizopungua MB 494. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Movies za kutafsiliwa GUSA HAPA>>>>
Real Moto

Kama ni wewe ni mpenzi gemu za mashindano ya pikipiki basi real moto linaweza kuwa bora sana kwako. Game hili huchezwa bila kutumia data yaani ni gemu la Offline. Limechezwa na zaidi ya watu Milioni kumi(10). Utaweza kutunza kumbukumbu zote za gemu hilo kwenye email yako ili simu ikipotea uendelee kucheza palepale ulipoishia kucheza gemu hilo pindi utakapopata simu nyingine na kuiingiza email yako.
Gemu hili hupatikana playstore kwa MB 143. Unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
Garena Free Fire

Garena Free Fire linatumia data na lipo hivi; Unamchagua mtu wako utakaemchezesha kisha unatupwa katika eneo moja na wenzako 49 wanaocheza gemu hilo muda huo duniani ili mupigane na uwemzima. Kwaiyo kila mtu utakaemuona katika gemu hili ni mtu anaepambania maisha na anaecheza kama wewe.
Zaidi ya watu Milioni 500 ulimwenguni wanalicheza Gemu hili kupitia vifaa vyao vya Android. Ni gemu linalopendwa na watu wengi kutokana na kuwa dogo kuliko magemu mengine ya muundo huu ambayo ni PUBG na CODM.
Unaweza kulipakua katika playstore kwa MB 674 pia unaweza rahisisha upatikanaji wake kwa kugusa INSTALL
Battle Of Agents: Gemu kuchezwa na watu wawili au zaidi bila data/internet GUSA HAPA>>>
Rarry Fury: Extrime racing

Kama unapenda gemu za magari usiache kupakua gemu hili lenye utofauti mkubwa na magemu ya magari yanayotamba kila mwaka. Game hili ni moja kati ya magame yanayopendwa na watu na mpaka Sasa limepakuliwa na zaidi ya watu Milioni 50. Linauhalisia wa kufurahisha wa mashindano ya Rarry.
Ukiachilia mbali muonekano wa game hili kuwa mzuri pia game hili linawezwa chezwa na mtu mmoja Offline au zaidi ya moja Online.Lina chukua kama MB 120 kulipakua na linapatikana katika playstore. Unaweza lipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
eFootball

Ukiongelea gemu kali za mpira wa miguu katika mwaka huu huwezi acha game hili. Gemu hili limepakuliwa na watu wengi sana hapa duniani na hii ni kwasababu liko vizuri. Kama umeshawahi cheza magemu ya PES basi tambua kuwa “eFootball” ni lile lile PES ila wamebadilisha jina tu.
Linachezwa Online na inashauriwa kuwa na mtandao usiosumbua ili uweze kulifaidi gemu hili bila usumbufu.Hupatikana playstore kwa GB 1.6 pia unaweza kulipata kirahisi sana kwa kugusa INSTALL
Simu ikiingia maji unatakiwa kufanya nini? GUSA HAPA>>>
Real Boxing
Hili ni gemu la mchezo wa ngumi ambalo mpaka sasa limechezwa na watu wasiopungua Milioni 10 ulimwenguni. Lipo vizuri sana kwanzia muonekano hadi sauti za vitasa(Ngumi). Kama ni mpenzi wa magemu ya kupigana, usikubali kuliacha gemu hili maana ni gemu lenye uhalisia wa mchezo wa kupigana wa Boxing.
Inashauriwa anaecheza game hili asiwe na miaka chini ya kumi na sita (16+). Game la Real Boxing hupatikana playstore kwa kama MB 291 ivi na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
Jumanji: Epic run

Kama unaijua vizuri filamu ya Jumanji au gemu la Tempo Run basi unaweza kulipenda zaidi hili gemu maana limeundwa kutokana na filamu ya Jumanji na muundo wake unafanana na gemu maarufu liitwalo Tempo Run.Ni gemu ambalo hujezwa bila data na mpaka Sasa linachezwa na zaidi ya watu million 10 duniani. Mchezaji wa gemu hili anatakiwa kuwa na umri usiopungua miaka 12.Linapatikana playstore kwa MB 154 na unaweza kulipata kirahisi kwa kugusa INSTALL
3 thoughts on “Magemu mazuri ya kucheza kwenye simu (Android)”
Comments are closed.