Mahusiano ya mapenzi huitaji vitu hivi

1. Ujasiri
Upendo unahitaji uwe jasiri katika hali zote ujasiri katika kunena ,ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.

2. Uvumilivu
Upendo unahitaji uvumilivu kuvumiliana. Hakuna mwanadamu aliyekamilika katika mambo yote, unajua Waswahili wanasema “mvumilivu hula mbivu “ mvumilivu katika upendo maana yake hii ni shule ya kila siku, tunajifunza kutokana na makosa. Uvumilivu unatakiwa sana katika upendo – unajua kumfanya mwenzi wako kuwa kama wewe unavyotaka awe inahitaji uvumilivu. Hilo ni kweli, maana mmetoka mazingira tofauti na malezi tofauti; hivyo kumbadilisha inahitaji uvumilivu.

3. Kiasi
Kiasi ni kitu muhimu. Chochote kinachofinywa zaidi ni hatari, unatakiwa uwe na kiasi katika mambo yako ili uweze kudumu katika upendo maana upendo unahitaji kiasi. Usijifanye uko (busy) sana unakosa hata nafasi/muda wa kukaa na mwenzi wako, lakini wewe unarudi usiku, huo sio upendo. Nakuombea uwe na kiasi ili uenzi katika maisha yako.

4. Kutiwa moyo
Upendo unahitaji kutiwa moyo. Mtie moyo mwenzi wako ukimwambia pole asali wangu wa moyo, Unafanya vizuri sana, umefanya vizuri sana, unapoweza kumtia moyo mwenzi wako kwa yale anayofanya yanamuhamasisha kutenda zaidi na kukupenda zaidi. Kutiwa moyo ni kufarijiwa, moyo unahitaji kutiwa moyo, kuthaminiwa. Hivyo katika upendo unahitaji kumtia moyo mwenzi wako ili upendo huo udumu maishani mwako. Ikiwa hauna tabia ya kumtia moyo mwenzi wako ipo siku utampoteza, akipata watu wanaothamini mambo anayoyafanya na kumfariji. Atulie badilika uuteke upendo kwa kufuata masharti yake.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

5. Kutambuliwa
Upendo unahitaji kutambuliwa katika maisha yako na kujua umuhimu wake. Kutambuliwa ni kitu muhimu sana katika maisha, kumtambua mpenzi wako na umuhimu wake kwako. Atambulike toka moyoni mwako kuwa anafaa kuwa mumeo au mke wako, hivyo upendo unahitaji sana utambuliwe na wewe mwenyewe. Umfahamu na umuelewe kiundani.

6. Uaminifu
Upendo unahitaji uaminifu kwa mwenzio sio msaliti wenye kujitunza na kujiheshimu mtu asiye na hila ndani yake uaminifu ni dawa ya upendo katika maisha yetu tukikosa uaminifu sisi kwa sisi upendo hautaweza kukaa pamoja nasi.

Gusa Hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

7. Usawa
Upendo unahitaji usawa unajua mapenzi ni kusaidiana hakuna kiongozi wa mapenzi bali tunasaidiana hivyo huo ndio usawa katika mapenzi upendo unahitaji usawa huo wewe unawajibu kwa mwenzi wako na mwenzi wako anawajibu kwako.

8. Urafiki
Upendo unahitaji urafiki upendo hujenga urafiki mwenzi wako ni rafiki yako kuliko marafiki ulionao katika maisha yako- Mapenzi wako sio adui yako mficha siri wako usimuogope maana upendo hauna hofu unatakiwa kuzungumza na rafiki yako kirafiki ili upendo uwezo kudumu na kushamili.

9. Kukubalika
Upendo unahitaji kukubalika, kupokelewa toka moyoni mkubali mwenzi wako apate kibali moyoni na maishani mwako ukimkubali hautamuumiza hivyo upendo unataka kukubalika hapo utafurahia maisha yako.

10. Ukweli
Upendo unahitaji ukweli,upendo ni adui wa uongo unatakiwa uwe mkweli katika mapenzi yenu,ukweli hujenga upendo, ukweli huimarisha mahusiano,upendo unahitaji mtu ambaye ni mkweli kwa mwenzi wake,ukweli ndio upendo wenyewe unatakiwa uwe mkweli ili upendo uchukue nafasi moyoni mwako.

11. Imani
Upendo unahitaji imani na imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ,ni bayana ya mambo yasio onekana. Unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako, imani katika mahusiano ni muhimu sana kuaminiana ,toa wasiwasi kwa mwenzi wako, mwamini kuwa amekuchagua wewe na hakuna mwinginen wewe uko peke yako.

Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO

12. Penzi
Upendo unahitaji penzi la kweli linalotoka moyoni ,penzi kwa mpenzi wako ni muhimu sana kama litatumika kwa utaratibu na kwa uaminifu kabisa maana penzi linahitaji muda hivyo hivyo unatakiwa uwe na muda wa kutosha ili uweze kupata pendo la kweli.