SUKARI YA DADA 05 🔞



Dah wakati Suzy akiendelea kutukana mtu kwenye simu yake mimi nilikua nawaza kuwa “Suzy ni mwanamke mzuri sana ambae nampenda na kumtamani mno ingawa naficha lakini ipo siku nitashindwa kujizuia, sasa sijui itakuaje yakinitokea ya huyu jamaa dah” nilikua nikiwaza hivyo kwasababu nilikua mmoja wa watu wanaoogopa kukataliwa na wanaowapenda.
Baada ya suzi kumaliza kuongea na simu, alirudi kukaa na mimi kwaajili ya kumaliza chakula chake lakini wakati huo alikuja na simu yake kabisa na alianza kula huku akiwapigia watu mbalimbali nisio wajua na mazungumzo nilioyasikia yalikua yanahusu biashara tu maana niliskia akiongelea vitu kama kutumiwa mahesabu, kuagiza mizigo mipya ya nguo zakike na zakiume toka china na kutaja viasi vikubwa vya pesa ambavyo kila nilipokua nikimuangalia nilikua naona ni vikubwa kuliko hata yeye mwenyewe. Kuongea kwake na simu kulimfanya aweanakula taratibu mno yaani mimi nilimaliza chakula nikawa nimekaa tu namuangalia lakini yeye alikua bado kabisa kumaliza na ameiweka simu sikioni anaongena na mtu huku anachota vijiko vya chakula kwa vituo vituo ili apate nafasi ya kutoa maneno. Basi Mimi nilikua natumia wakati huo kumuangalia sura yake nzuri jinsi alivyo barikiwa lipsi na macho mazuri makubwa kiasi pia niliangaza nilikua nikitupa macho kifuani pake nilikua naviona vitunda kama msumari vimilivyojitokeza kwenye nguo lainii aliokuakaivaa.
Mwisho alimaliza kuongea na simu akaiweka mezani na aliona Mimi nipo tu mbele yake nimemaliza kula lakini soda ipo pembeni na sijaifungua mpaka muda huo. Aliniambia “Duh umemaliza kula chakula mimi bado tu”

“Hahaha lakini wewe si ulikua unaongea na simu”

“Haha,yaah biashara hizi zinasumbua kweli.. ila tekinolojia imenirahisishia kidogo mpaka naweza kuseti mambo nikiwa nyumbani tu ingawa siku mojamoja inabidi ukakague mambo yanaenda vipi”

“Mh alafu sijawahi kutana na mtu kama wewe tangu nizaliwe yani?”

“Kwanini?” Alijibu akiwa na wasiwasi kuwa nitazungumzia kuhusu kutojihusisha na wanaume

“Yaani sijawahi kutana na binti rika yako alafu anaongea vitu vikubwa kama unavyo ongea wewe”

“Hahahaha kawaida sana Bwana.. vipi mbona hunywi soda?”

“Mh sijisikii tu, hamu imekata ghafla eti”

“Duh au nikuletee juisi maana kuna juisi kwenye friji nilitengeneza leo asubuhi.. sjui utaipenda?”

“Hapana achananayo, nisikusumbue tu”

“Hunisumbi Bwana… Ngoja nikakuchukulie” Alinyanyuka na kuichukua soda yangu kisha akaelekea kwenye friji kuirudisha soda na kunichukua Juisi. Baada ya muda alirudi na Juisi ikiwa kwenye glasi kisha akanipa alafu akaendelea kula chakula chake..
Nilimwambia “Asante” akajibu “powa” kisha nikanyanyua glasi na kuinywa kidogo. Sijui upendo tu nilionao kwake, maana nilona Juisi ni Tamu sana mpaka nikijikuta namuuliza “Ivi hii Juisi ulisema umetengeneza wewe?”
“Ndio nimetengeneza mimi, kwani ni vipi?”
“Inaonekana unajua sana kutengeneza Juisi maana hii Juisi ni Tamu sana”
“Hahaha kawaida mbona” na kupitia uso wake niliona aibu zilimuingia kidogo kisha akatabasamu kutokana kumsifia kwangu yaani alikua kama ameanza kulainika kiasi tofauti kabisa na nilivyo tarajia. Niliongeza kwa kumwambia “Ukawaida unauona wewe… tena huwenda ni kwasababu umezoea kutengeneza vitu vizuri” alicheka “hahaha” lakini wakati alipokua akimaliza tu kucheka, ziliskika kelele za geti likijifungua na hii ilikua ni ishara kwamba kuna gari inaingia. Suzy alishtuka ghafla na kuropoka kwa kisauti cha chini cha hofu “Mama huyo amekuja!” alafu akabeba chakula chake,sahani yangu na soda yake haraka na kukipeleka jikoni kisha akatoka jikoni na kupitia simu yake iliokua mezani akielekea haraka haraka katika vyumba vya kulala kisha nikasikia akiubamiza mlango “Mbaah!!!”. Baada ya sekunde chache mama yake aliingia na kunikuta niko kwenye meza ya chakula nimekamata glasi ya Juisi akaniuliza “Vipi, dada yako amekupa chakula?
“Ndio amenipa.. Asante Sana”
“Anha usijali.. Kwaiyo yeye yuko wapi?”
“Yupo.. alielekea vyumbani huko”
“Mh litoto hili yaani limeona shida mpaka kukaa na kaka yake hapa.. mhm” alafu nae akaanza kuelekea huko huko vyumbani na kuniacha pale nikiwa nawaza “kwanini Suzy amejiondoa haraka karibu yangu aliposikia mama yake anakuja wakati mama yake anataka ajisogeze kwa wanaume?”…

INAENDELEA…

Unataka tukutumie simulizi nzima kwa njia ya WhatsApp? GUSA HAPA

One thought on “SUKARI YA DADA 05 🔞”

Comments are closed.