SUKARI YA DADA 04 🔞

Nilijibu “Sawa” lakini kiukweli uongeaji wake ulikua ni wakujiamini kama mwanaume mpaka nikajiuliza kimoyo moyo “Mh Sawa amenichanganya lakini nitamuingiaje huyu?” lakini nilijipa moyo huwenda Penzi linaweza mbadilisha…
Kwa muda huo niliamua kumchukulia jinsi alivyo yaani ingawa alikua akiuvutia moyo wangu lakini nilikua naongeanae kama mwenzangu tu. Alinionesha sehemu nyingi za nyumba hiyo na alikua akinielekeza namna gani natakiwa kufanya ili kumfurahisha mama yake ambae ndio bosi wangu pia alinigusia kidogo kuhusu swala la ukali wa mama yake, alisema mama yake ni mkali mno na ukali wake huongezeka mara dufu pale mtu anapomjibu wakati amechukia hivyo niwe makini sana katika hilo. Katika maongezi nilijaribu kuanza kumchimba kuhusu ugomvi wao na mama yake kwa kumuuliza “Ivi kwanini mmekua kama hampatani na mama yako?”
Lakini cha ajabu aliyakatisha maongezi kwa kunijibu “Ndio hivyo bigi.. huwa hatupatani tu. Nafikili sehemu zote nimeisha kupitisha, twende ndani basi ukale chakula maana bi mkubwa ndio huyoo anaondoka na gari, na huwa hakawi kurudi tena akikukuta hujala ataongea sana”
Nilipoangaza nikaona gari getini ikisubiri geti la Automatic lijifungue ili liweze kutoka na ndani ya gari hilo alikuwemo mamaake Suzy ambae ndio mama mwenye nyumba mwenyewe lakini hiyo haikua sababu tosha ya kutonijibu kwa undani swali langu ila sababu ilikua ni kwamba hataki kabisa kuvizungumzia vitu vinavyo muhusu yeye.

Basii tuliingia ndani akaniacha kwenye sehemu ya kulia chakula kisha akaingia jikoni na kurudi na chakula sahani mbili, akanipatia moja kisha akavuta kiti na kukaa na mimi mezani ili na yeye ale chakula chake kilichokua kwenye sahani. Mimi na yeye tulianza kula tukiwa katika meza moja tena tumegeukiana huku macho yangu yakimtazama kila mara maana alikua ananivutia sana lakini yeye alikua hana hata dalili ya kuniwaza yaani alikua busy mno. Baada ya yeye kula vijiko kadhaa nilimuona akinyanyuka nakuelekea sehemu ambayo kulikua na friji, skujua alikua anaenda kufanya nini lakini nikakuta tu akirudi akiwa na soda mbili aina ya pepsi katika mikono yake huku ameining’iniza Opener katika kidole chake kwaajili ya kufungulia soda hizo… Alifika katika meza na kuniambia “Sorry hapa huwa tunatumia soda za pepsi tu hivyo kama utapenda unaweza ukawa unashushia hii” huku akiisogeza soda moja upande wangu pembeni kidogo na chakula nilichokua nakula kisha akatumia Opener kuifungua soda yake “Chisiii..!!!!!” Alafu akaiweka Opener hiyo kwenye uso wa meza na kuisukuma ili ije kwangu kwa kujibuluza kwenye meza lakini kwa bahati mbaya ilijibuluza kwa kasi mpaka mwisho wa meza wa upande wangu na nilishindwa kuizuia mpaka ikadondoka chini “Ndingiritiii..!!!!” Nikamsikia akisema “Ooh Sorry” nikamjibu “haha usiwaze Suzy” kisha nikainama chini ya meza ili kuiangalia na kuiokota. Niliona lakini wakati nikiwa nimeinama chini ya meza nikitaka kuichukua nilitupa macho kwabahati mbaya upande aliokaa Suzy, nilichokiona kiliniduwaza kidogo maana nilikua nikiona asilimia kubwa ya mwili wa Suzy ulivyo umbika. Niliona mguu pamoja na paja nene zilizokua ziking’ara kutokana na usafi wake yaani mazingira tu yalionesha kuwa yaliyomo yamo tena niliyatamani mno. Wakati nikiendelea kuyazubalia hayo ghafla niliskia ya Suzy sauti juu ya meza “Vipi hujaiona?” Mh nilishtuka nikanyanyua kichwa bila umakini nikajikuta nimejigonga chini ya meza “khuuuh!” nikasika sauti ya Suzy juu ya meza ikisema “Oh.. Oh.. pole” mungu akasaidia nijichomoa vizuri chini ya meza na kuja juu haraka kisha nikamjibu “Dah.. Asante” huku nikihema mno na kwa muda huo niliduwa pia Suzy alikua ananiangalia usoni lakini mimi nilikua nakwepesha macho kwa kuangalia pembeni, juu na chini kutokana na aibu za kujishtukia kitu nilichokua nikikifanya chini ya meza. “Fungua soda sasa.. mbona umeshikilia Opener alafu hufungui soda wala huendelei kula?.. umeumia au?” Nilimsikia Suzy akiniambia hivyo huku akiwa na sura ya wasiwasi kidogo baada yakuniona nimeganda tu mbele yake bila mimi mwenyewe kujitambua lakini niliposikia hivyo tu, akili ikarudi na nikamjibu kwa kumzuga “Nipo Sawa.. ila nilikua najiskia kizungu zungu kidogo” alitabasam kidogo kisha akasema “Anha sawa.. endelea kula basi”.


Basi nikaendelea kula na hamu yote ya soda ilikata pia yeye aliendelea kula lakini wakati tukiendelea kula iliskika simu ikiita kwenye meza ya TV. Basi nilimuona Suzy akinyanyuka kuifuata na Kama kawaida yangu, macho hayakuacha kulicheki zigo la Suzy lililokua likijitikisa vilivyo.

Niliendelea kushuhudia Suzy akiipokea simu aina ya iPhone ilikua ikiita kisha nikamsikia suzi akifoka “Sasa wewe mpumbavu baada ya kunitumia mimeseji yako ya Mapenzi usiku kucha umeamua munipigia mi mama ako?… Acha ujinga fuata yako mbwa wewe!!!”
Akuishia hapo, bado nilimsikia akiporomosha matusi makubwa makubwa ambayo yalikua yananitetemesha mpaka mimi maana pamoja na kwamba sikusikia na sauti ya aliekua akiongeanae lakini maneno ya Suzy yalionesha wazi kuwa anaongea na mwanaume mwenzangu aliekua akijaribu kutupa nanga kwa bibie Suzy.

Dah wakati Suzy akiendelea kutukana mtu kwenye simu yake mimi nilikua nawaza kuwa “Suzy ni mwanamke mzuri sana ambae nampenda na kumtamani mno ingawa naficha lakini ipo siku nitashindwa kujizuia, sasa sijui itakuaje yakinitokea ya huyu jamaa dah” nilikua nikiwaza hivyo kwasababu nilikua mmoja wa watu wanaoogopa kukataliwa na wanaowapenda…

INAENDELEA…

Unataka tukutumie simulizi nzima kwa njia ya WhatsApp? GUSA HAPA

One thought on “SUKARI YA DADA 04 🔞”

Comments are closed.