
Nilijiweka Sawa kisha nikasogelea chumba cha bafu ambacho kilikua kinasikika kelele za maji yakitiririka mwilini mwa Tausi lakini ghafla kabla sijaingia ndani yake niliskia kishindo kizito sana ndani ya bafu “Mbuuh!!” kikiambatana na “Mamaaaah!!!”. Nilishtuka sana na nikaamua kuufungua mlango kwa nguvu ilikujua nini kilichomtokea Tausi. Nilimkuta Tausi akiwa amelala chini tena kalalia Sura akiwa hana nguo yoyote katika mwili wake na maji yakiendelea kumwagika chini na kuchanganyikana na damu iliokua ikimwagika kutoka maeneo ya kichwa chake. Nilimfuata haraka kisha nikamnyanyua na kumpeleka moja kwa moja katika kitanda. Alikua amelegea mno kama mtu alielala usingizi mzito alafu alikua na mchubuko mdogo uliokua ukitoka damu nyingi kiasi katika sehemu ya paji la uso. Kutokana na mazingira, nilishindwa hata kuomba msaada maana ilikua ni usiku wa kama saa 8 ivii na pia nilikua na hofu kubwa ya binti huyo kupoteza maisha na mimi kuingia matatizoni.
Nilifungua begi langu na kuchomoa moja ya T-shirt zangu nyeupe pendwa na nikaitumia kuukandamiza mchubuko wake kwa sekunde kadhaa ili kufanya damu zisiendelee kutoka. Mungu alisaidia, damu ilikata kabisa lakini dalili za kuamka zilikua hakuna kabisa ingawa nilikua nikimshtua mara kwa mara kwa sauti ya chini “Tau.. Tausi.. amka basii.. amka rafiki yangu! Tau mama! nionee huruma.. amka basi” huku moyo wangu ukidunda mithiri ya mlio wa Generator na jasho likinishuka mno…
Nilikua nasikiaga tu kuwa Usiku ni mfupi sana kama mtu uko kwenye matatizo lakini siku hiyo niliamini kwakua nilikuta saa1 asubuhi imefika kwa haraka sana na bado Tausi hajaamka.. Niliendelea kujifungia kwenye chumba hicho huku nikiwa na hofu kama mtu aliekojoa ugenini lakini baada ya muda niliskia mlango ukigongwa “Ngo, ngo, ngo” nilishtuka na hofu iliongezeka mpaka nikaanza kutetemeka huku mlango ukiedelea kugongwa “Ngo,ngo,ngo”.

Dah nilifikilia jinsi ya kufanya nikaona kufungua mlango inaweza kuwa ni uamuzi mbaya kwangu kwasababu hata mtu asipoona kinachoendelea ndani, akiiona sura yangu tu atagundua ninamatatizo makubwa hivyo niliamua kumfokea kwa sauti kali na ya juu yule mtu aliekua anagonga mlango “Unagonga!.. Unagonga!… Unagongagonga milango asubuhi yote hii, watu tunakula raha zetu wewe unaleta usumbufu.. Tatizo NinI!?!??!? Ehee!?!??” Baada tu ya kufoka hivyo niliskia sauti ya kikohozi kidogo ikitoka karibu yangu “khooh!” nilipoangalia vizuri nilikuta ni Tausi ndie alikua akikohoa baada ya kurudishwa fahamu na makelele yangu. Baada ya kuona hivyo sikuwa na muda tena wa kusikiliza majibu ya mtu wa mlangoni mpaka akaondoka mwenyewe. Nilimchangamkia Tausi ili kujua anaendeleaje, anajiskia vipi na anahitaji nini na kwa wakati huo aliniambia anahisi njaa.. bila kupoteza muda nilitoka nje nakumtafutia chakula cha haraka kisha nikarudi kumpatia. Alikula na nikaendelea kuongea nae mambo mengi sana ili kuirudisha kumbukumbu yake na muda huo ndio niliutumia kumuazima simu yake kisha nikawasiliana na wenyeji wangu ili waje kunichukua kwenye Guest hiyo. Tausi alinishukuru kwa kuokoa maisha yake na alinipatia namba yake ya simu nikaiandika katika karatasi ili niweze kuonana nae kwa mara nyingine kisha akaondoka na kuniacha nikisubiri mwenyeji wangu kuja kunichukua.
Baada ya muda mfupi nilichukuliwa na deleva wa pikipiki alietumwa na wenyeji wangu kisha nikashushwa kwenye mjengo wa kifahari ambao ninaenda kufanya kazi ndani yake. Mjengo ulikua na wigo mkubwa sana na nilipoingia nilipita kwenye bustani kubwa sana ya maua kabla ya kuifikia nyumba yenyewe. Nilifika kwenye mlango na kuugonga mara kadha “Ngo ngo ngo” “Ngo ngo ngo” baada tu ya kumaliza kugonga nikasikia sauti ya mama ambae nilihisi kuwa ndie mama mwenye nyumba akimfokea biti yake ndani “Ivi wewe inamaana, huo mlango unaogongwa huusikii au?!.. huo upumbavu wako ndiomaana kila siku nakwambia tafuta mume uniondokee we hutaki! na huo uzuri wako, utazeekea hapa hapa mbwa wee! kafungue mlango huko!”
INAENDELEA…
Unataka tukutumie simulizi nzima kwa njia ya WhatsApp? GUSA HAPA
One thought on “SUKARI YA DADA 02 🔞”
Comments are closed.