1) USILIBEBE KAMA VILE NI TATIZO KUBWA SANA. lichukulie kama tatizo la kawa ida ili uipe akili yako nafasi ya ku relax na kupata maarifa mapya.
2)WAWEKE WAZI MARAFIKI ZAKO NA WAKE. unapokuwa wazi kuongea unakuwa unatoa ile sumu ya uchungu moyoni, na wanaweza wakakupa faraja. Lakini ukikaa nalo moyoni unaweza ukafa siku si zako kwa presha!
Gusa hapa>> USOME JAMBO ZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO
3)USIPENDE KUTEMBELEA AU KUFANYA VITU AMBAVYO MLIKUWA MNAFANYA PAMOJA ENZI HIZO. hiyo inaweza ikakuzidishia maumivu na kumkumbuka.
4)USIANZISHE MAHUSIANO MAPYA HARAKA HARAKA. jizuie kuanzisha mahusiano mapya haraka kama vile njia ya kumsahau coz unaweza ukajikuta unapata mtu ambae atakuumiza tena ukazidi kujiona una mkosi.
5) USIMWAMBIE MPENZI WAKO MPYA MABAYA YA MPENZI WAKO WA ZAMANI. Usimwambie mabaya ya mwenzie anaweza akajiona yeye ndio malaika na hivyo akakunyanyasa kwa kukumbushia aliyokuwa anakufanyia mwenzie. Mwelezee mazuri ya mwenzie ili atamani kukutendea mazuri zaidi.
