STORI ZA VICHEKESHO ZINAZOWEZA KUKU VUNJA MBAVU


STESHENI YA TRENI

Jamaa wawili walifika stesheni wakakuta tren ndo kwanza inaondoka. Wakaanza kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondoka…

Yule Aliye baki akaanza kucheka sanaa
Mpaka machozi yakamtuka. Watu wakamuuliza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu:
“Kinacho nichekesha , yule aliye panda alikuwa ananisindikiza.

GUSA HAPA>> KUPATA VITU VIZURI ZAIDI KWAAJILI YAKO SASA


NDEGE ILIOPATA AJALI

Ndege ilipata hitilafu angani Ndipo rubani akatoa taarifa kwamba ndege imepata hitilafu na itadondoka baada ya dakika 10. Ndani ya ndege kulikuwa na watu watano Lakini maparashuti yalikuwa manne tu.
Watu hao ni mchungaji, waziri, mwanajeshi, Msukuma na mwanafunzi wa chekechea, Mchungaji akasema yeye anategemewa na kanisa hivyo hapaswi kufa. Akachukua parachute akaruka. Waziri akasema wananchi wanamtegemea alete maendeleo, Akachukua parachute akaruka. Msukuma akasema familia inamtegamea akachukua parachute akaruka faster.
Wakabaki mwanajeshi na mwanafunzi wa chekechea. Yule mjeshi akamtazama mwanafunzi akamuonea huruma kisha akasema. Mimi najitolea kufa kwa ajili yako, we chukua hilo parachute lililobaki ujiokoe halafu mi ntakufa na hii ndege.
Yule mwanafunzi akajibu “usijali yamebaki maparashuti mawili” yule mjeshi akashangaa akauliza mawili kivipi.? Mwanafunzi akasema YULE MSUKUMA KACHUKUA BEGI LANGU LA SHULE ALIDHANI NI PARASHUTI


NAMBA MPYA

Mke wangu alisajili line mpya jina la Jenifer Godson bila mimi kujua.
Jana usiku nimerudi home akaniomba elfu 10 akasuke.
Nikajibu sina elfu 10 nikampa buku 4
Wakati tumelala, Mara Paa msg katika simu yangu

“HI MY LOVE”.

Kidume nikatoka nje nikaenda toilet, nikaijibu:
“we nani”

MSG: ni mimi Jane Msambwanda”.

Kusikia Msambwanda, mshipa wa ubongo ukanicheza.
MIMI: Jane Msambwanda wa wapi tena?”

MSG: Bwana baby nawe, si pale unapokulaga kila siku?”

MIMI: “ooh, kumbe unaitwaga Jenifer, namba yangu umeipata wapi?

MSG: “nimepewa na rafiki yako DJ Tipwil, nakupenda sana handsome, sema huwa naogopaga kukwambia, ila mi sijiwez juu yako, yaani kila ukija kula, natamani usiondoke, nikwambie yaliyomo moyoni mwangu, nateseka sana mwenzio”

MIMI: Jamani pole mpenzi, hata mimi nilikuwa nakupenda, yaan kila nikiona huo msambwanda nahisi mzunguko wa damu kubadilika, I love you too honey.

MSG: Basi mpenzi ,nikuombe kitu

MIMI: aah, sema tu

MSG: naomba elfu 50

MIMI: nakutumia sasa ivi”
(NIKATUMA)

MSG: Waaoo asante mume wangu, haya rudi ndani tulale, mi mkeo MAMA KIDUKU hapa..

πŸ™†β€β™‚πŸ™†β€β™‚πŸ™†β€β™‚

🎼_hapo ndo utaukumbuka wimbo wa dunia Lukumba lukumba🎼


KITOTO KIJINGA

WAGOGO watatu walisafiri, walipofika kwa ndugu yao mjini wakapewa soda wakasemezana GALIMUZINZI, Yaani tamu, walipoondoka mmoja alitia kizibo(cha kisoda) mfukon badae walipotoka nje akamnong’oneza mwenzie MUYANGU NASOLA MBEYU! Yaani, mwenzio nimechukua mbegu nikapande.


HUU NDIO UBAYA WA KUWA NA MWALIMU MKUU ALIESOMEA SAYANSI

*MWALIMU: Nani alimuuwa Chifu Mkwawa?
Mwanafunzi 1; Sio mimi
Mwanafunzi 2: Jana sikuja shule
Mwanafunzi 3:Mwalimu kwa kweli sie unatuonea….baada ya mwalimu kuona darasa zima ni vilaza akaamua kumtaarifu mwalimu mkuu, ambaye naye akaja kwa ukali
MWALIMU MKUU: Nani aliyemuua Chifu Mkwawa? Msipojibu humu ndani patawaka moto…darasa zima wakaanza kulia
Darasa:Mwalimu sio sisi
Mwalimu Mkuu akamgeukia mwalimu wake akamuuliza, “Mwalimu una uhakika huyo muuwaji yuko darasa hili?” πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚


KITAMBULISHO CHANGU

NLKUA NATEMBEA NKAONA MWENDAWAZIMU AKIOKOTA NOTI YA KSH.1000 MBELE YANGU.
MIMI: samahani sana boss, hio uliookota hapo ni kitambulisho changu.
MWENDAWAZIMU: hatakama cjui kitambulisho lakini hiki si kitambulisho, OK Kama ni kitambulisho chako kweli nambie waitwa Nani? Na umezaliwa mwaka gani
MIMI: naitwa JAMHURI KUU YA KENYA na nimezaliwa mwaka wa 1000.
MWENDAWAZIMU: oh Pole boss kwa kukupotezea wakati shika kitambulisho chako, lakini mbona uko na vitambulisho vingi na unavibwagabwaga ovyoovyo? Nko na vyengine ishirini hapa acha nkupe mwenyewe.
MIMI: asante sana kwa kuniokotea izo ni photocopy na nimuhimu sana kwangu. Zilipotea tangu mwakajana zinanpatia shida sana.